Jifunze kufikiri kuhusu maisha yako ya mbele yatakavyokuwa na kuchukua hatua SASA (be proactive). Kwa kufanya hivyo unaweza kuepuka baadhi ya matatizo yasikupate. Hutakuwa hivyo ulivyo siku zote. Mfano, itakuwaje ukishindwa kufanya unalofanya sasa, ukistaafu, ukiondoka katika cheo hicho, wanaokupendelea wakiondoka au wakibadilika, ukiachia gari la ofisi nk.
Kuna hadithi moja ya mfanyakazi wa benki
ambaye aligundua kwamba anaachishwa kazi kwa kosa alilofanya. Akatafakari jinsi
ambavyo hana uzoefu wa kulima wala kuwa ombaomba. Alichofanya ni kujitafutia
marafiki kabla hajafukuzwa kwa kuamua aingie hasara katika kile ambacho
angepata kama faida. Usisubiri uishiwe pesa ndipo utafute marafiki. Nakuambia,
watakukimbia na kushindwa kupokea simu zako! Anza kuwatafuta sasa wakati una
chochote hata kama hakikutoshi wewe mwenyewe. Uwe na siku njema.
Lawi Mshana