Ticker

6/recent/ticker-posts

Be an example by apologizing to your child (Uwe mfano kwa kumuomba mwanao msamaha)

Video link: Uwe mfano kwa kumuomba mwanao msamaha

Be an example by apologizing to your child

(Uwe mfano kwa kumuomba mwanao msamaha)

We often do not listen to our children and teenagers. As parents or caregivers, we usually see ourselves as always right, so we struggle to apologize.

A certain teacher beat a student, claiming he had stolen his pen. While beating him, the student said, "But you have put the pen by your ear!" Since the teacher did not want to appear wrong, he replied, ‘I did not mean this, but the other one.’ 

When you make a mistake, even if you are an adult, you should apologize. By doing so, you teach the child that when a person makes a mistake, they should ask for forgiveness.

Uwe mfano kwa kumuomba mwanao msamaha

Mara nyingi hatuna usikivu kwa watoto na vijana wetu. Tunajiona kama wazazi au walezi kama tuko sahihi wakati wote hivyo hatuwezi kuomba msamaha.

Mwalimu fulani alimchapa mwanafunzi akimtuhumu kwamba amemuibia kalamu. Wakati anamchapa mwanafunzi akamwambia mbona kalamu umeiweka sikioni! Kwa vile mwalimu hakutaka aonekane kwamba amekosea, akamjibu akisema, ‘Sina maana ya hii bali ile nyingine.’

Unapokosea hata kama ni mtu mzima unapaswa kuomba samahani. Kwa kufanya hivyo unamfundisha mtoto kwamba mtu akikosea anapaswa kuomba msamaha.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Mentor, +255712924234, Tanzania