Know God’s purpose more accurately
(Jua kusudi la Mungu kwa usahihi zaidi)
God uses all things to bring good to our lives. You are so special to Him. Rom 8:28 “We know that all things work together for good for those who love God, to those who are called according to his purpose.”
When Joseph was sold by his brothers, he chose to be ‘better’ instead of becoming ‘bitter’. Gen 50:20 “As for you, you meant evil against me, but God meant it for good, to bring to pass, as it is this day, to save many people alive.”
You are indeed very committed to serving God. However, something is missing in your life. Work on it! Acts 18:24-26 “Now a certain Jew named Apollos, an Alexandrian by race, an eloquent man, came to Ephesus. He was mighty in the Scriptures. This man had been instructed in the way of the Lord; and being fervent in spirit, he spoke and taught accurately the things concerning Jesus, although he knew only the baptism of John. He began to speak boldly in the synagogue. But when Priscilla and Aquila heard him, they took him aside, and explained to him the way of God more accurately.”
Put everything to the test before believing and applying it in your life. Acts 17:11 “Now these were more noble than those in Thessalonica, in that they received the word with all readiness of the mind, examining the Scriptures daily to see whether these things were so.”
Know the character of your spiritual leaders. 2 Tim 3:14 “But you remain in the things which you have learned and have been assured of, knowing from whom you have learned them.”
Jua kusudi la Mungu kwa usahihi zaidi
Mungu hutumia vitu vyote kuleta mema katika maisha yetu. Wewe ni wa pekee sana Kwake. Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
Yusufu alipouzwa na ndugu zake, alichagua kuwa ‘bora’ badala ya kuwa ‘mchungu’. Mwa 50:20 “Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.”
Ni kweli kwamba umejitolea sana kumtumikia Mungu. Walakini, kuna kitu kinakosekana katika maisha yako. Kifanyie kazi! Mdo 18:24-26 “ Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”
Jaribu kila kitu kabla ya kuamini na kukitumia maishani mwako. Matendo 17:11 “Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.”
Jua tabia za viongozi wako wa kiroho. 2 Tim 3:14 “ Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao.”
Dr. Lawi Mshana, Facilitator & Mentor, +255712924234, Tanzania