ACHA MISIMAMO AMBAYO MSINGI WAKE SIO BIBLIA BALI NI MAPOKEO
YA KIDINI NA KIBINADAMU ILI USIJE UKAPOTEA MILELE!
Tumeagizwa kurejeza watu kwa upole na sio kwa mashindano
wala mabishano kama tunaongozwa na Roho Mtakatifu. Gal 6:1 “Ndugu zangu, mtu
akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama
huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe
mwenyewe.”
Kuna mambo mengi ambayo tunafanya lakini hatupendi KUHOJI
kama chanzo chake ni Mungu, shetani au mapokeo ya dini zetu. Mungu atatumia
Biblia katika kuhukumu wanadamu. Mshitaki wetu ambaye ni shetani naye atatumia
Biblia hiyohiyo kama alifanikiwa kukupotosha mahali fulani ukamtii. Ufu 12:10
“Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na
ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini
mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na
usiku.”
MIONGONI MWA MASWALI MUHIMU TUNAYOTAKA KUPATA MAJIBU YAKE
1.
Unawezaje kuibiwa vipawa na mafanikio yako kwa kufanya uzinzi au uasherati?
2.
Unawezaje kutupwa katika moto wa milele kwa kuota ndoto mbaya?
3.
Unaweza kuikosa mbingu kwa kutumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango?
4.
Kwanini utahukumiwa kwa kuangalia picha za utupu (ponografia) na kupiga
punyeto?
5.
Biblia imetofautishaje wanaume na wanawake katika kutoa huduma za kiroho?
6.
Ni sawa kuchangia na kushiriki sherehe zenye vileo, miziki ya kidunia na uvaaji
wa kipagani?
7.
Kwa nini Mungu atawahukumu watu wanaotoa sadaka na zaka katika makanisa potofu
ambayo yanaongozwa na watumishi wa uongo?
8.
Kwanini wanandoa watahukumiwa kwa kutolipa mahari hata kama ndoa imefungwa
kanisani?
9.
Je bado Mungu wa Agano Jipya anataka uitakase siku yako maalum ya ibada?
10.
Kwa nini mtu anahukumiwa kwenda motoni kwa kufanya mambo mabaya ambayo hakujua
kwamba ni dhambi?
11.
Wanandoa wanawezaje kuhukumiwa kama wazinzi wakati hawajatoka nje ya ndoa zao?
12.
Kwa nini mkristo anaweza kupoteza nafsi yake kwa kuvaa vito (madini) katika
mwili wake?
13.
Kwanini Mungu anawahukumu watu kwa kutomwabudu Yesu Kristo peke yake?
14.
Kwanini Mungu atawahukumu watu wanaovaa mavazi yanayokosesha wengine?
15. Kwanini utahukumiwa kwa kuabudu mahali ambapo dhambi haikemewi hata kama wewe binafsi unajitahidi kuacha dhambi?
Waebrania 2:1-3 “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.”
Mungu atusaidie tumuone Yesu mbele yetu na sio mapokeo ya wanadamu ambao ni wapitaji tu katika dunia hii. Yohana 12:21 “…. sisi tunataka kumwona Yesu.”
Maswali haya yanajibiwa katika group la Facebook la MAISHA YA MKRISTO WA KWELI
Lawi Mshana, +255712924234; Tanzania