Ticker

6/recent/ticker-posts

KIFO SIO DHARURA HIVYO TUJIANDAE TUNAWAACHAJE WENGINE


 KIFO SIO DHARURA HIVYO TUJIANDAE TUNAWAACHAJE WENGINE

Hivi karibuni tulikuwa kwenye mkutano wetu wa mwaka wa Beyond Four Walls ambapo pamoja na mambo mengine tumekumbushana kuhusu kujiunga na bima kwa ajili ya kifo. Baadhi ya wanachama wa BFW ni wanachama pia wa kikundi cha bima kwa ajili ya kushikwa mkono mwanachama akifariki au akifiwa na mwenzi, watoto, wazazi au wakwe.

Ingawa tunachangia sherehe nyingi kwa mwaka, tunaona vigumu kujiwekea kiasi hiki kidogo kwa ajili ya misiba. Matokeo yake tunaaibika au tunaishi maisha magumu sana baada ya kufiwa kwa sababu ya madeni au kulemewa na gharama za misiba.

Wiki hii tutalipa ada ya mwaka huu ambapo wanachama wapya wanaweza kujiunga na kikundi chetu ambacho kimesajiliwa benki. Kikundi hiki kina wanachama wa dini zote (Wakristo na Waislamu) maana kifo hakina dini.

Mchango wako unategemea unataka bima iguse familia yako tu au pamoja na wazazi/wakwe zako. Mchango wako kuanzia TZS 12,000 hadi 72,000 kwa mwaka unaweza kusaidia ufutwe machozi ukifiwa au familia yako ifutwe machozi wewe ukitangulia mbele za haki. Malipo utakayopata kwa mchango wako mdogo ni kati ya 600,000 na 5,000,000 kulingana na mchango wako na aliyefariki ni nani (mwanachama au mwenzi wa mwanachama, mtoto, mzazi nk)
Hivi karibuni imani iliongezeka wanachama walipoona mwenzao aliyefiwa na baba mzazi akipokea TZS 1,000,000 (milioni moja).

Shirika letu linajengea uwezo jamii ishinde uhatarishi, umasikini na utegemezi kwa kutumia mbinu shirikishi. Ndiyo maana tunakujuza jambo hili muhimu kwa maisha yako na familia yako. Kila uchao tunaona watu wakifariki na Mungu ameweka wazi kwamba hii ndiyo njia ya kuondokea duniani kwa wote ambao unyakuo hautawakuta wakiwa hai.

Hivyo hatuna sababu ya kuwaacha watu na vilio vya kimaisha vinavyoepukika. Nimeshuhudia watu wengi wanapofariki, wakiwemo viongozi wa dini, watu wakililia MAISHA YATAKUWAJE kuliko KUONDOKEWA NA MPENDWA WAO! Tusipuuze jambo hili.

Zaburi 90:10 “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.”

Karibu sana

Dr Lawi Mshana, 0712924234, Korogwe, Tanga