Ni jambo la baraka sana kuona Watanzania tunakuwa
wafadhili kwa ajili ya mahitaji ya watu wanaoishi mazingira hatarishi. Mama
kutoka Morogoro ameguswa na huduma hii na kuamua kutoa nguo zake. Nimepokea
mzigo huu leo. Naamini Mungu hatanyamaza bali atakutana na haja za moyo wake
kwa jinsi ya kipekee sana.
Bilashaka hata wewe una vitu ambavyo huvitumii kwa sasa
ambavyo vingesaidia katika huduma na ofisi zetu za kujengea uwezo jamii na
kusaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na majanga kv nguo, viatu, vitabu, vyakula,
fanicha, kompyuta, bajaji, gari nk.
Dhamira ya shirika letu ni kutumia mbinu shirikishi
katika kukabili utegemezi na umasikini kuliko kutegemea wafadhili kutoka nje
peke yake. Ni kweli tunahitaji misaada kutoka nje lakini kuna mambo mengi
ambayo hata sisi tunaweza kuyafanya. Sisi pia tunahitaji baraka zinazopatikana
kwa kusaidia WANYONGE. Mdo 20:35 “Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi
hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema
mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.”
Waumini wengi watapoteza roho zao milele bila kutenda dhambi zilizozoeleka duniani kama vile wizi, uzinzi nk. Wengi hawajui kwamba kutojali kutimiza mahitaji ya wasiojiweza ambayo tunayamudu kunatosha kutupeleka motoni. Mungu atusaidie sana tuuelewe ukweli huu. Mt 25:41-16 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”
Karibu sana ushiriki katika utumishi huu au utuunganishe na fursa unazozijua.
Dr. Lawi Mshana, Beyond Four Walls (NGO),
+255712-924234