MUNGU
HAKUKUSUDIA WANANDOA WAISHI KAMA WAPANGAJI
Wakati pekee ambapo katika uumbaji Mungu alisema SI VEMA
au HAJAFURAHI ni pale alipoona Adamu ni mpweke. Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke
yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
Leo tuna wanandoa wengi wanaoishi kama wapangaji – yaani wanaishi
pamoja lakini kila mmoja ana mipango yake, malengo yake na maono yake. Hawa wamevaa
tu koti la ndoa lakini ni wapweke (married singles).
Mungu anataka ndoa iwasaidie wanandoa kuukabili upweke (married
couple) – yaani watoke kwa wazazi (waanzishe mfumo mpya wa maisha yao), waambatane
(wawe na mambo yanayowaunganisha) na ndipo watakuwa mwili mmoja (watakamilishana
badala ya kutofautiana). Mwanzo 2:24 “Kwa
hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja.”
Msikilize Mwinjilisti Minja (mama Mchungaji Lawi) na timu
yake wakisema na wewe.
Kama wanandoa tunashirikiana katika huduma za semina na makongamano
kwa vile tunaamini ndoa ni wajibu mkubwa katika ufalme wa Mungu na sio nyumbani
peke yake. Wasiliana nasi.
Kumbuka ku-follow ukurasa na ku-subscribe kwenye channel
yetu.
Dkt. Lawi Mshana, +255712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania