Ticker

6/recent/ticker-posts

Mambo 12 wanayoomba waabudu shetani kila siku

MAMBO KUMI NA MBILI WANAYOOMBA (AU WANAYOTAMKA) WAABUDU SHETANI KILA SIKU – Lawi Mshana 1. Kwamba Mpinga Kristo aje kabla Kanisa halijajiandaa. 2. Kwamba watumishi, viongozi na wamishenari waanguke. 3.Kwamba huduma na kazi za Bwana ziharibike. 4. Kwamba Wakristo watosheke na hali waliyo nayo, watafute makanisa ambayo hayahubiri Injili kamili na watafute wachungaji wanaotafuta amani kuliko ukweli. 5. Kwamba Wakristo waache kufunga na kuomba. 6. Kwamba Karama za Roho zipuuzwe. 7. Kwamba familia na ndoa zivunjike. 8. Kwamba wachungaji, watumishi, na viongozi wa Kanisa wagombane na kupambana. 9. Kwamba pasiwepo umoja wa kweli wa wachungaji na makanisa. 10. Kwamba wachungaji na viongozi wapigwe magonjwa na ulemavu ili washindwe kuendelea na huduma. 11. Kwamba kizazi kijacho kiangamizwe na kisifikie hatima waliyokusudiwa na Mungu. 12. Kwamba Kanisa lisiwaachilie na kuwaandaa watu kufikia kusudi lao la ki-Mungu. Kumbuka, wanaombea faraka iwepo na umoja bandia uwepo ili waweze kuiharibu imani ya kweli. Ushuhuda: Mkristo fulani alikuwa akisafiri kwa ndege. Alipoona jirani yake aliyekaa naye karibu anaomba kwa juhudi akamwambia, “Naomba tushirikiane katika maombi”. Akamjibu sawa. Hitaji tunaloombea muda huu ni ndoa za Wakristo zivunjike. Ndipo Mkristo huyo alipogundua kwamba kumbe sio mwenzake. Katika safari zangu za ndani na nje ya nchi nimegundua kwamba kuna waabudu shetani makanisani kuliko tunavyofahamu. Ni pale tu tutakapofanya maombi mazito katika Jina la Yesu Kristo na damu yake ndipo tutawabaini na kuwasaidia kuwa huru na sisi wenyewe kuwa salama. Dr Lawi Mshana, Korogwe, Tanga, Tanzania