Ticker

6/recent/ticker-posts

Mungu anakupenda

Pengine unapata mshtuko unaposikia mtu akikuambia, Mungu anakupenda. Unajiuliza, ‘Mungu angenipenda angeruhusu haya yote yanipate?’. Nataka leo nikuhakikishie kwamba Mungu anakupenda na anakujali sana. Hebu jiulize haya maswali yafuatayo: 1.Pamoja na matatizo haya ninayopitia, mbona nimefikiwa na ujumbe huu kwamba Mungu ananipenda? 2.Mbona kuna watu wenye matatizo makubwa kuliko ya kwangu lakini hawajakata tamaa kama mimi? 3.Mbona wengine ambao hawakuwa na matatizo kama mimi wameshafariki dunia? 4.Mbona bado kuna watu wananithamini na kutaka kuongea na mimi? 5.Mbona ninapoacha kuwaza matatizo yangu ninaanza kupata amani moyoni? Ndugu yangu mpendwa, Mungu anakupenda kwa upendo wa milele. Yer 31:3 “Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.”. Anakupenda hata kama humfanyii chochote. Katika mpango wake, alipenda na wewe uwepo duniani. Analo kusudi maalum na wewe. Wapo wengi waliokuwa na matatizo makubwa lakini wakaguswa na upendo wa Mungu. Mfano: 1.Mtu aliyetengwa na jamii kwa sababu ya ugonjwa wake. Marko 1:40-42; 5:25-34 “Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.” Marko 5:25-29 “Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.” 2.Mtu aliyetumikishwa na dhambi. Yohana 4:16-18, 21-26 “Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”. 3.Mtu aliyehukumiwa kuuawa baada ya kukamatwa akitenda maovu. Yohana 8:3-9 “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.” 4.Mtu aliyetaka kujiua kwa hofu ya hukumu yake. Matendo 16:25-31 “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.” Amua leo kumpokea Yesu Kristo ili uuone wema wake. Zab 34:8a anasema, Onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema. Kama uko tayari kumpokea Yesu sasa, omba hivi kwa moyo wako wote: Ee Bwana Yesu, nakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi. Naliitia Jina lako. Nisamehe dhambi zangu zote. Naamini ulikufa kwa ajili yangu. Naamini ulifufuka kutoka kwa wafu kama yanenavyo maandiko. Nakupokea katika maisha yangu uwe Mwokozi wangu binafsi. Asante Yesu kwa kuniokoa. Amen. Kama umeomba sala hii kwa kumaanisha kabisa, UMEOKOKA LEO. Unachotakiwa kufanya ni kuanza kusoma Biblia, kumwomba Mungu na kushiriki ibada katika kanisa lenye mafundisho sahihi ya kibiblia linaloamini kwamba tunaokolewa tukiwa hapahapa duniani. Wokovu sio tukio (event) la mara moja tu bali ni mchakato (process) hadi tutakapofikia hatua ya kutukuzwa (glorification). Rum 8:30 “Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Hata wewe ambaye hujafikia uamuzi wa kumpokea Yesu leo, bado ni wa thamani kwetu na kwa Mungu. Mungu anaweza kutatua shida zako zote za kibinafsi, za ndoa yako, familia yako na hata ukoo wako. Wasiliana nasi leo kwa ajili ya kufundishwa, kushauriwa na kuombewa ili uwe huru kweli kweli. Rev Dr Lawi E. Mshana Box 554 Korogwe, Tanga, Tanzania Cel: 0712-924234 Fax: 027-2640520 Email: mshanalawi@gmail.com