Hatua za kukuwezesha kufikia hatima yako Na. 8: Unakwenda wapi? (Steps to achieve your destiny No. 8: Where are you going?)
John 10:10 “The thief comes only to steal and kill and destroy; I have come that they may have life, and that they may have it more abundantly.” The final question to ask yourself is, ‘What is your Canaan?’ To know where you have arrived, you must know in advance where you are going. You may work and do business, but you do not know who you want to be. If you do not ask yourself this question, you are doing your work just to make a living. As a result, you have a good salary or income but are burdened with debt. Many of us like to buy things that cost us money (liabilities) instead of starting with things that generate income (assets). You must know the path that will take you to your Canaan and make a contribution to your community.
Hatua za kukuwezesha kufikia hatima yako Na. 8: Unakwenda wapi?
Yn 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Swali la mwisho la kujiuliza ni, ‘Kanani yako ni ipi?’ Ili ujue umefika mahali, lazima ujue mapema kwamba unaenda wapi. Unaweza kufanya kazi na biashara lakini hujui unataka uwe nani. Kama hujiulizi swali hili unafanya kazi zako kwa ajili tu ya kujikimu. Matokeo yake unakuwa na mshahara au kipato kizuri lakini umelemewa na madeni. Watu wengi tunapenda kununua vitu vinavyowagharimu (liability) badala ya kuanza na vitu vinavyoingiza kipato (asset). Lazima ufahamu njia itakayokufikisha katika Kanani yako na kuwa na mchango katika jamii yako.
Kwa uwezeshaji wa warsha, tafadhali kuwa huru kuwasiliana nami (For workshop facilitation feel free to contact me):
Dr Lawi Mshana, +255712924234 Tanzania


