TAMBUA NA KUITUMIA VIZURI NEEMA
KATIKA MAISHA YAKO
Maono: Nilisikia ujumbe ukisema, Neema inatufundisha
kukataa ubaya. (Ikabidi nilitafute hili andiko na kulisoma vizuri)
Tito 2:11-15 “Maana neema ya Mungu
iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa12 nayo
yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate
kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini
lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;14 ambaye alijitoa nafsi
yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe
milki yake mwenyewe, wale walio na
juhudi katika matendo mema.15 Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote;
asikudharau mtu awaye yote.”
Vipengele vya maombi
1. Neema ya wokovu ifunuliwe kwetu – Hii neema ni zaidi ya kusema, Nimeokoka. Neno ‘wokovu’ limebeba mambo mengi (holistic) kv wokovu wa roho, uponyaji, mafanikio, kurejezwa, kuhuishwa nk. 2 Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.”
2. Tufundishwe kukataa ubaya (ungodliness) na tamaa za dunia (wordly lusts) – tuwe na tabia za Uungu. 2 Petro 1:4 “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.”
3.
Tuwezeshwe kuishi kwa kiasi (soberly), haki (righteous) na utauwa katika
ulimwengu huu wa sasa (godly in the present age)
Tito 3:14 “Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.”
4. Tuweze kutazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu
1 Yohana 3:2,3 “Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.”
5. Tutambue
kazi ya Yesu msalabani (kujitoa kisadaka, kutukomboa na maasi yote, kutusafisha
tuwe milki yake [wenye juhudi katika matendo mema] )
Ebr 12:2 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.”
6. Tuwe jasiri na kujituma katika utumishi bila kuogopa watu
2 Timotheo 2:1 “Basi wewe, mwanangu, uwe
hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.” Mithali 29:25 “Kuwaogopa
wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye Bwana atakuwa
salama.”
Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania