VIFUNGO VINAVYOZUIA KUWALETA WATU KWA YESU
1. UJINGA (IGNORANCE) I Peter 3: 15 Tutaendaje wakati hatujui cha kusema, tutumie mbinu gani na jinsi ya kujibu maswali ya wapinzani?
2. HOFU (FEAR): 2 Tim. 1:7; Lk. 9:26 Kuna sababu nyingi za hofu kv hofu ya kukataliwa na marafiki, umasikini, kukosa elimu nk
3. KUTOAMINI (UNBELIEF): Eze 3:18-20 Huamini kwamba unaweza kwenda motoni kwa kutojali uinjilisti. Mdo 20:26 au kukunyima taji mbinguni Dan 12:2,3
4. IBADA YA SANAMU (IDOLATRY, MATERIALISM) Mhu. 3:1, Kujali mambo yetu na kusahau misheni yetu tuliyopewa mf biashara zetu, kazi zetu, familia zetu, masomo yetu nk. Ufu 21:8
5. MATESO KUTOKA KATIKA FAMILIA ZETU, MARAFIKI, JAMII, SERIKALI NK. Efe 6:6; Ukinunua kitu mpe na kipeperushi. 1 Pet 2:4
6. KUAHIRISHA AU KUCHELEWA (PROCRASTINATION OR DELAY) Yn 4:35 Kumbuka mtu anaweza kuwepo kesho akaondoka kesho. Mfanyakazi anaweza kuwepo leo kesho akahamishwa. 2 Kor 6:2
7. UDUNIA (WORLDLINESS) Mt. 6:19-21 Unawaza sana fasheni, sherehe, safari zisizo na maana, tamthilia mpya, mitandao ya kijamii nk 1 Yoh 2:17; 2:15
8. MARAFIKI WABAYA (BAD COMPANY): I Kor. 15:33, Mit. 13:20 Kujenga urafiki wa karibu na wasioamini bila kuwashuhudia au waliorudi nyuma.
9. KUSHINDWA (FAILURE OR DESPAIR): Fil. 3:14 Unaweza kualika watu wasije kanisani nk 2 Kor 4:8-11
10. KUKOSA HURUMA (LACK OF COMPASSION): Mt. 9:36, Omb. 1:12. Huduma ya Yesu ilitanguliwa na huruma.
11. USHUHUDA ULIOHARIBIKA (DESTROYED TESTIMONY): Mt. 5:13-16 Sisi ni chumvi tukiharibu ushuhda na uadilifu hatutakuwa na ufanisi. Tusikwepe kodi, tusiuze vitu ambavyo si halali, tuwalipe wahudumu wetu mishahara, tusinung’unikiwe na wateja wetu nk.
12. KUPENDA DHAMBI (THE LOVE OF SIN): II Pet 2: 18-22 Kumpenda mwenzi au watoto kuliko Mungu, kupenda kufunga ndoa na mtu ambaye hajaokoka nk.
13. SHETANI NA NGUVU ZA GIZA I The. 2:18, Mdo 13:6-12; 16: 16-20; Ufu. 12:12 Shetani ni adui mkubwa wa Injili.
Dr Lawi Mshana, +255712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania