KAZI YA NENO LA MUNGU
1.
Kututoa katika maangamizi
Zab 107:20 “Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.”
2.
Kutusaidia kujua kusudi la Mungu
2 Kor 12:6-10 “Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu. Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.”
3. Kutakasa
na kusafisha Kanisa
Efe 5:25-27 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.”
4. Kuokoa
watu na kuwaandaa kuwa watumishi wa Mungu
Yn 4:28-30,38-39 “Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, 29 Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? 30 Basi wakatoka mjini, wakamwendea. 38 Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.39 Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.”
Ufunuo – nikiwa katika maombi usiku wa kuamkia leo
Tuwe waangalifu isije ikatupasa adhabu
pamoja na dunia kwa kushindwa kumtii Mungu kwa kuwaleta watu kwa Yesu na
kuwafanyia uanafunzi. 1 Wakorintho 11:32 “……
isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.” Kama tungewaambia watu kuhusu
MATENDO MAKUU ANAYOTUTENDEA MUNGU, wangemkimbilia na kumwamini.
Wiki iliyopita nilifunuliwa kwamba Kanisa linaishi katika laana kwa sababu ya kumtumikia Mungu kwa ulegevu. Shetani anatumia andiko hili kudai haki yake ya kutesa Kanisa kimaisha. Yeremia 48:10a “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu.”
Tukumbuke kwamba tunapaswa kutumia muda wa Mungu vizuri. Zaka (fungu la kumi) la muda wa Mungu kwa siku (masaa 24) ni takriban masaa mawili na nusu. La kusikitisha hata siku ya Bwana Jumapili bado tunafanya mambo yetu na katikati ya wiki muda wote tumetingwa na kazi zetu binafsi.
Maombi
1. Ee Mungu nisaidie nitambue kwamba
nina ole kwa kutofanya kazi yako kama ulivyoniita.
2. Ee Mungu naomba unirehemu na
kunisamehe. Usiniadhibu kama unavyoiadhibu dunia isiyokujua.
3. Ee Mungu naomba unisaidie nitambue
kazi na nguvu ya Neno lako na nisiweze kunyamaza bila kuwajulisha wengine ukuu
wako.