MWALIKO WA KIPINDI CHA WATOTO/VIJANA WA DINI ZOTE
Washiriki: Watoto
na vijana (adolescents and youth) kuanzia umri wa miaka 10 hadi 24
Wapi: Ukumbi wa
Hema (TLMC) karibu na Magereza – Manundu kati (Korogwe mjini)
Lini: Jumapili
tarehe 25 Juni 2023
Muda gani: Saa
9.30 alasiri
Mada: Stadi za
maisha za kushinda vishawishi na uhatarishi
Kwanini: Watoto
na vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi nyumbani, mtaani wakienda na kutoka
shule, shuleni, mtandaoni na wanapotembelea jamaa na marafiki.
Waandaaji:
Nitatoboa Initiative (mpango wa malezi ya vijana balehe na vijana wadogo)
unaoratibiwa na shirika la Beyond Four Walls, Korogwe, Tanga.
Mzazi na mlezi tunakuomba umruhusu kijana ashiriki kipindi hiki ili
kumlinda dhidi ya changamoto nyingi zinazomkabili ukizingatia ni kipindi cha
likizo na ni wikiendi.
Beyond Four Walls ni shirika lisilo la kiserikali linalojengea uwezo
jamii ishinde uhatarishi, utegemezi na umasikini kwa kutumia mbinu shirikishi.
“We look at Tanzanian youth as potential partners, rather than just as
beneficiaries.”