KWA NINI UNATOA SADAKA LAKINI MAISHA YANAZIDI KUWA MAGUMU (Bofya hapa uangalie video)
KWA
NINI UNATOA SADAKA LAKINI MAISHA YANAZIDI KUWA MAGUMU
Utangulizi: Lazima tutambue kwamba mkulima havuni vizuri kwa
sababu tu amepanda mbegu. Mkulima mwenye busara anazingatia kanuni za msingi kv
udongo, msimu, mbegu, matunzo ya shamba nk
Watu wa Mungu wengi wanajiuliza kwanini ni waaminifu katika utoaji lakini maisha yanazidi kuwa magumu. Kumbuka hapa nazungumzia mtu kubarikiwa na kuwa na muda na Mungu na familia yake. Unaweza kuwa na baraka nyingi lakini huna muda na Mungu (bali ni bidii yako mwenyewe) au baraka hizo hazitoki kwa Mungu.
1. Toa kwenye madhabahu sahihi – epuka kujiunganisha na madhabahu za manabii wa uongo na wachawi. Kama ulishajiunganisha hakikisha unajitoa ktk madhabahu zao na sio kuhama dhehebu tu. Muombe Mungu akuongoze ukatoe wapi na ukaabudie wapi hata kama ni mbali.
Kum 12:13 “Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; bali katika mahali atakapopachagua Bwana katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo.”
2. Hakikisha sadaka inatumika kwa ajili ya Ufalme wa Mungu – sadaka hizi haziteketizwi bali zinatumiwa kwa kazi za kanisa. Je unaridhika kwamba kazi ya Mungu inafanyika hapo au watu wanajitajirisha tu?
Luka 8:5 “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.”
Zingine zilianguka kwenye mwamba, zingine kwenye miiba na zingine kwenye udongo mzuri (hizi zilizaa 60 na 100).
3. Panda mbegu na sio mavuno – kuna watumishi hakuna siku wanakuhamasisha na wewe ujenge nyumba au biashara yako ikue. Wao ni michango ya kanisa tu mwaka mzima.
Usipande mavuno na usile mbegu! Niliwahi kuanzisha “operesheni kakae kwako”. Yeremia 29:5 “Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake.”
2 Wakorintho 9:10 “Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu.”
4. Zingatia uwiano wa mbegu na mavuno unayotaka kupata – Mkulima anayetaka magunia 50 anazingatia ukubwa wa shamba na wingi wa mbegu. Mungu hafanyi mazingaumbwe.
Kama hujawahi kumpa Mungu zaidi ya michango ya sherehe na misiba, sahau kupokea mambo makubwa kutoka kwa Mungu.
2 Wakorintho 9:6 “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.”
5. Fahamu msimu mzuri – usipande wakati wa kiangazi
Zekaria 10:1 “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.”
6. Usitoe sadaka pamoja na watu ambao umejiridhisha kwamba kipato chao kinatoka katika madhabahu za shetani. Mungu hana shida ya pesa, anahitaji moyo mkunjufu na fedha ya halali.
Hosea 4:14 “Sitawaadhibu binti zenu wazinipo, wala bibi arusi zenu wafanyapo uasherati; maana wao wenyewe huenda kando pamoja na wanawake wazinzi, hutoa dhabihu pamoja na makahaba; na watu hawa wasiofahamu wataangamia.”
Unapojua chanzo cha kipato cha mtu kuwa sio sahihi, unapaswa kuepuka. Mfano, pesa kutoka kwa wachawi.
7. Toa sadaka yenye thamani kwako – usiangalie washirika wengine wanavyotoa. Angalia kiwango chako cha maisha
Malaki 1:8 “Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema Bwana wa majeshi.”
Ushuhuda:
1. Mimi nina kiwango cha chini cha kutoa
kila ibada. Kama sikwenda ibada kadhaa, siku nikienda natoa zote. Je ukiwa
mpangaji hulipi kodi unaposafiri mwezi mzima?
2. Mimi ninatoa zaka ya kila ninachopata. Kama ni vigumu nathaminisha na kutoa zaka yake. Pengine unatoa zaka ya pesa tu lakini ukipewa nguo hutolei zaka.
Tangu nifanye hivyo nimewezeshwa kufanya vitu vikubwa bila kuwa ombaomba, tegemezi wala kulemewa na madeni.
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuchukua hatua baada ya
kusikia ujumbe huu ili nipokee baraka kutoka kwako.
KWA USHAURI NA MAOMBI UNAWEZA KUWASILIANA NAMI KWA SIMU
NAMBA 0712-924234