Ticker

6/recent/ticker-posts

MUNGU AMEKUNYANG’ANYA TALANTA KWA VILE HANUFAIKI NA WEWE (Video na Maandishi)

MUNGU AMEKUNYANG’ANYA TALANTA KWA VILE HANUFAIKI NA WEWE  (Bofya hapa uangalie video)

MUNGU AMEKUNYANG’ANYA TALANTA KWA VILE HANUFAIKI NA WEWE

Ndoto: Nimeona watu wakinyang’anywa karama kwa vile hawazitumii. Kisha akapewa anayezitumia kwa faida.

1. Ufunuo wa Yohana 3:11 “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.” Tambua umepewa nini halafu jifunze kulea na kukitumia ulichopewa.

Mt 25:27-29 “basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.”

Mungu hajawahi kumbariki mtu ambaye hajui ANA NINI – Musa, una nini mkononi? Mwanamke mjane – una nini nyumbani kwako?

2. Mt 3:8-10 “Basi zaeni matunda yapasayo toba; wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

Acha kujivunia dini, dhehebu, huduma ya kiongozi wako nk – jali wewe mwenyewe kuzaa matunda.

3.   Yohana 15:2,8 “Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.”

Unaweza kuwa tawi lililoondolewa na huna habari; tawi lizaalo Mungu analiprune zaidi. 

4.  Mk 11:12-14, 20-22 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia. Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.”

Unaweza kulaaniwa kama Mungu anapohitaji kitu kwako hapati. Yeremia 48:10a “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu.”

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba unisaidie nitambue talanta yangu na kuitumia kuzalisha kama ulivyonipa uwezo.

2. Ee Mungu naomba unirehemu na kuondoa laana yoyote inayonikwamisha katika maisha yangu.