BADO JAMII HAITAMBUI UZITO WA KAZI YA WALIMU NA WAHUDUMU WA AFYA
Leo tulikuwa
na muda wa kupitia matokeo ya tathmini ya awali kwenye shule ya sekondari
ambayo wanafunzi wake walishiriki katika mahojiano hapa Dodoma Jiji.
Tulithibitisha uhatarishi uliotajwa na wanafunzi ili tujue namna
tutakavyotafuta ufumbuzi wa kudumu.
Lakini walimu
pia wana changamoto nyingi. Jamii inamtarajia mwalimu afanye zaidi ya matarajio
bila kujali kwamba na yeye ana mahitaji ya msingi katika kuboresha mazingira
yake ya kazi na ya familia. Hakuna wakati mwalimu akikosea anachukuliwa kama ni
bahati mbaya. Pamoja na kujitolea kufundisha muda wa ziada bila malipo, bado
jamii haitambui kwamba amejitolea. Mwalimu anaweza kufokewa mbele za watu bila
sababu za msingi.
Tunahitaji
kuwajali walimu tukizingatia kwamba wana muda mwingi na watoto wetu kuliko sisi
wenyewe kama wazazi.
Ungana nasi
katika mpango wetu wa kutambua kazi njema wanayofanya walimu na wahudumu wa
afya kama makundi ambayo jamii inaona mapungufu yao tu na kusahau mazuri wanayoyafanya.
Dr Lawi
Mshana, Beyond Four Walls, 0712-924234


