SIKU YA TATU YA ZIARA YETU YA KUTHIBITISHA UHATARISHI SHULENI
– DODOMA JIJI
Tunashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa ambao tumeendelea
kuupata kutoka kwa walimu wakuu na walimu waliokaa kikao na sisi. Naamini baada
ya zoezi hili tutakuwa tumepata uhalisia wa changamoto ambazo ziko ndani ya
uwezo wa shule na zile ambazo zinahitaji kuungwa mkono na wadau wengine katika
kuzitatua.
Tunaamini walimu pia wana changamoto nyingi ambazo
zinahitaji kupatiwa ufumbuzi. Kuna wakati tunasahau kwamba hata walimu wanatoka
katika familia hivyo wanahitaji pia malezi na matunzo.
Ungana nasi katika huduma hii ukizingatia kwamba watoto wetu
wako muda mwingi zaidi shuleni kuliko nyumbani na katika nyumba za ibada.
Dr. Lawi Mshana, Beyond Four Walls NGO, +255712924234