KIKAO CHA ‘KIKOSI KAZI’ CHA KUANDAA MKAKATI WA KUKABILIANA NA UHATARISHI - DODOMA
Katika kikao chetu cha kutoa matokeo kuhusu ripoti ya tathmini
ya awali (needs assessment report) tulikubaliana tuwe na kikosi kazi chenye
wajumbe kutoka kila mtaa kwenye kata tunayofanya kazi hapa Jijini Dodoma.
Leo tumekutana kuthibitisha uhatarishi ulioainishwa na
kuweka mkakati wa namna tutakavyoukabili tukishirikiana na serikali na wadau wa
maendeleo. Lakini pia tumeanza kukutana na walimu kwa ajili ya mkakati wa kufanya
kazi pamoja kukabili uhatarishi mashuleni.
Tunahitaji sana msaada wako wa kuunga mkono juhudi hizi ili
vijana balehe na vijana wa nje ya shule wawe salama shuleni, njiani, nyumbani
na katika nyumba za ibada.
Wasiliana nasi sasa!
Dr Lawi Mshana, Beyond Four Walls, 0712924234 (Simu na
Whatsapp)





