Ticker

6/recent/ticker-posts

HUWEZI KUSHINDA UTUMWA WA MADENI BILA KUPATA ELIMU SAHIHI (sikiliza somo kuhusu KUKOPA, BAJETI NA MATUMIZI)

KUKOPA, BAJETI NA MATUMIZI (Bofya hapa)

HUWEZI KUSHINDA UTUMWA WA MADENI BILA KUPATA ELIMU SAHIHI (sikiliza somo kuhusu KUKOPA, BAJETI NA MATUMIZI)

Maswali ya kujiuliza:

·       Unajua tofauti ya KANUNI na SHERIA za Mungu?

·       Unajua Mungu alisema nini kuhusu kukopa katika Neno Lake?

·       Unajua wenye kipato kikubwa wamelemewa na madeni kuliko wanaoishi maisha ya kawaida?

·       Unajua wewe huna mpango thabiti wa dharura na hata pesa ikiongezeka hakuna mabadiliko yoyote yanayotokea katika maisha yako?

·       Unajua huna mwongozo wowote kuhusu matumizi ya pesa zako na hujui ni vitu gani vinakula zaidi pesa zako?

·       Unajua asilimia ya kipato chako unayotakiwa kutumia kwa mahitaji mbalimbali kv matumizi ya nyumbani, usafiri, malezi, burdani, akiba nk?

Ushuhuda: Kuna kipindi katika familia yangu tuliamua kuandika kila kitu tunachonunua kwa mwezi mzima. Mwisho wa mwezi tulishangaa kugundua kwamba pesa nyingi sana imetumika kununulia sukari. Ilibidi tuulizane kama kuna watu wanalamba sukari maana kilikuwa kiasi kikubwa sana. Baada ya hapo tukaweka utaratibu wa kukabiliana na matumizi yasiyo ya lazima.

Hutaweza kufanikiwa kimaisha kwa kuombewa tu au kwa kumtolea tu Mungu kwa uaminifu. LAZIMA PIA UJIFUNZE KUWA NA MATUMIZI YALIYO YA LAZIMA NDIPO UTAKUWA NA MATOKEO MAZURI.

Tito 3:14 “Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.”

Nimetumia kanuni hizi kununua vifaa vya gharama, kujenga nyumba mbili, kusafiri safari za kimataifa nk bila kukopa wala kuwa ombaomba.

Tatizo la watu wengi wenye kipato cha kawaida ni KUANZA KUNUNUA VITU VINAVYOTUMIA PESA ZAO (LIABILITIES) BADALA YA KUANZA NA VITU VINAVYOWAINGIZIA PESA (ASSETS). HAWAJUI KWAMBA MATAJIRI WANAANZA NA ASSETS NDIPO WANUNUE MAGARI YA KIFAHARI (LIABILITIES). Wapo walionishangaa kwanini nimeanza kununua bajaji badala ya gari la kutembelea.  

Unaweza kuupata ujumbe huu bure ila unashauriwa kuchangia chochote kwa ajili ya huduma hii ili wengine nao wafikiwe pia. Hata hapa unapofikiwa na taarifa hii kuna mtu fulani amegharamia.

Hili somo lina urefu wa saa 1 na liko katika mfumo wa MP3 hivyo hata mwenye simu ndogo anaweza kusikiliza na kujifunza. Hata hivyo mtu anaposikiliza anatakiwa kunipa mrejesho ameguswa wapi na ameamua kuchukua hatua gani katika kubadili maisha yake.

Lakini pia natoa mafunzo haya kwa warsha na makongamano ili kuwasaidia watu wajitambue kwamba wanaweza kubadili maisha yao bila kuwa tegemezi wa mikopo na misaada.

Karibu sana.

Dkt. Lawi Mshana, +255712924234; Korogwe, Tanga, Tanzania