MUNGU
AKINUFAIKA NA WEWE, ANAJIBU HARAKA MAHITAJI YAKO BINAFSI
Usiku tukiwa katika maombi
nilipata ujumbe huu muhimu kwako unayetafuta sana upendeleo (favor) wa Mungu.
Tatizo lako unaombea na kutafuta sana ufumbuzi wa mahitaji yako ya kibinafsi na
kusahau kuombea mambo ambayo yanamgusa Mungu kwa haraka. Ukimgusa Mungu hawezi
kuacha kutimiza mahitaji yako hata kama hujamuomba. Hebu jiulize: Hivi Rais wa
nchi yetu akiona unamfaa, utakuwa na ulazima wa kumueleza shida zako binafsi?
1. Tafuta mafanikio ya kazi ya Mungu kuliko ya kwako binafsi
Maandiko yameweka wazi kwamba kama
unataka KUZIDISHIWA (kujibiwa mahitaji yako binafsi), UTAFUTE KWANZA UFALME WA
MUNGU NA HAKI YA MUNGU.
Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki
yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
2. Usijisumbue
sana na kusahau kwamba Mungu ndiye aliamua kukuleta duniani
Usijisumbue (usi-struggle)
sana na maisha bali jifunze kujikabidhi kwa Bwana alliyekuleta hapa duniani kwa
kusudi maalum. Anajua kwa nini alikuleta duniani. Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika
kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu.”
3. Hana
alipata watoto wake mwenyewe baada ya kuamua kuomba kwanza apewe mtoto kwa ajili
ya kazi ya Mungu.
Alipozomewa kwa kutozaa
alifika mahali akaamua aombe mtoto ambaye hatanufaika naye.
1 Sam 1:11 “Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa
majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala
usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo
mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe
hautamfikilia kichwani kamwe.”
Baada ya kumpata mtoto huyo
ndipo tumbo lake likafunguka kwa ajili ya watoto wake binafsi. 1 Sam 2:21 “Naye Bwana akamwangalia Hana, naye
akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo
mtoto Samweli akakua mbele za Bwana.”
Mungu ana majibu yako lakini
ufunguo wake ni kuhakikisha unatanguliza ufalme wa Mungu kuliko maisha yako
binafsi. Tangu wengine tugundue siri hii hatujapungukiwa.
Mwaliko
Tunajiandaa kumaliza mwaka
na kuanza mwaka mwingine. Huduma tunayofanya inagusa na kujengea uwezo jamii
bila kubagua dini wala dhehebu. Tunakualika uungane nasi kwa kujaza fomu ya kujitolea
kuwa rafiki-mwenza au mdau (partner) kwa mwaka 2025. Zipo huduma unazoweza
kuzifanya hata kama uko mbali nasi. Shiriki katika maono haya makubwa
yanayogusa ulimwengu mzima. Yapo mataifa ambayo haingekuwa rahisi kuyafikia
lakini kupitia huduma hii tumeweza kuyafikia.
Njia rahisi zaidi ni kuwasiliana
nasi ni kwa kupitia hapa kwenye tovuti (WASILIANA NASI) au baruapepe (info@lawimshana.com) au kupitia Whatsapp
(0712-924234).
Wewe ni mtu muhimu sana
kwetu.
Karibu sana
0712924234.


