Video: Karibu ushiriki maombezi kwa wasap bure
MWONGOZO WA KIPINDI CHA KLINIKI YA UPONYAJI
KITUONI NA MTANDAONI
Dr. Lawi Mshana
Kliniki ya uponyaji ni kipindi cha maombezi nje ya muda wa ibada za Kanisa ambacho ni maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo sugu ambayo yana udhihirisho wa wazi wa nguvu za giza.
Mtu anapohitaji huduma hii anapaswa kufanyiwa mahojiano ya kutambua uzito wa tatizo lake (diagnosis) na awe tayari kushiriki vipindi kadhaa mpaka atakapokuwa huru kwelikweli. Kuna wakati Mungu haponyi kwa MUUJIZA wa papo kwa papo bali anaponya kwa MCHAKATO (HATUA KWA HATUA). Anayefanyiwa huduma ataeleza mabadiliko anayoyapata mpaka atakapofunguliwa.
Andiko linaloongoza Kliniki ya Uponyaji ni Mk 8:22-26 “22 Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23 Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? 24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. 25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. 26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie.”
Andiko hilo linatufundisha kwamba kuna matatizo ambayo Mungu hayaondoi kwa TUKIO la muujiza wa papo kwa papo bali kwa MCHAKATO.
Kuna mambo
kadhaa ambayo yalifanyika kabla ya huyu mtu kuwa huru kwelikweli.
1. Yesu alimtoa
nje ya kijiji – alimtoa katika mazingira hatarishi
2. Yesu
alimwekea mikono – alimfanyia huduma ya uponyaji
3. Yesu
alimuuliza kama anaona kitu – alitaka kujua mabadiliko yaliyoanza kutokea
4. Yule mtu
alitazama juu – alifanyia kazi kile alichokuwa hawezi ili agundue kama amepona
5. Yule mtu alisema
anaona watu kama miti inayotembea – alieleza hali yake bila kuficha (alisema amepata
nafuu ila bado hajapona vizuri). Hakulazimishwa kukiri kwamba amepona.
6. Yesu
alimuwekea tena mikono yake – alipoona kwamba hajapona vizuri alimgusa tena
7. Yule mtu
alitazama sana akaona vizuri – alijitahidi kufanya anachoweza ili kuthibitisha kama
amepona ndipo akapona kabisa
8. Yesu hakumruhusu kuingia kijijini – hakuruhusiwa kurudi kwenye kile kijiji (pengine kilikuwa na maagano yaliyosababisha matatizo yake)
Kwa yule ambaye anaweza kufika katika kituo chetu anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Afanyiwe mahojiano ili kugundua uzito
wa tatizo lake – matatizo mengine yanahitaji aombewe kwenye vipindi vya maombi
vya kanisa au kwenye kikundi cha maombi. Hata hivyo lazima mhitaji (mteja)
apangiwe muda maalum (appointment) kwa vile ni huduma inayohitaji kuombea kwa
ufuatiliaji wa karibu na sio kuombea kundi la watu kwa pamoja.
2. Kama ana
sifa za kufanyiwa maombi katika kipindi cha Kliniki ya Uponyaji atatakiwa
kufanya yafuatayo:
·
Atatakiwa
kushiriki kipindi cha maombezi ya ufunguzi cha Jumatatu saa 4 asubuhi – kipindi hiki kimepangwa muda huu wa
asubuhi kwa sababu zifuatazo: Kuhudumia mhitaji aliyechoshwa na tatizo lake
kiasi cha kusimamisha kazi zake kama anavyofanya anapoenda hospitali, muda huu atahudumiwa akiwa
bado hajachoshwa na kazi zake binafsi, tutakuwa na muda wa kutosha kuombea,
kuhoji na kushauri kuliko jioni, ni muda wenye utulivu mkubwa kwa vile hata
wanafunzi wako mashuleni, hauingiliani na ibada za makanisani na wahitaji wanaotoka
mbali wataweza kuja na kurudi kila siku bila kikwazo.
·
Atatakiwa kuwa tayari kufululiza kwa siku kadhaa (hata hivyo baada
ya siku ya kwanza muda unaweza kubadilika kulingana na aina ya tatizo na nafasi
ya wahudumu.)
Atafanyiwa huduma katika
maeneo makuu manne – 1. Uponyaji
wa ndani
2. Kuangusha ngome 3. Kuondoa haki ya kisheria ya mapepo 4. Kutoa mapepo
3. Mhitaji atatakiwa kusindikizwa na ndugu wa karibu ili kusaidia dharura zikijitokeza (hasa kwa wenye mapepo au magonjwa yanayohitaji usaidizi wa karibu). Sio lazima huyo msaidizi wake ahusike katika vita vya kiroho. Anaweza kuwa nje na kuitwa pale dharura inapojitokeza.
4. Mhitaji asije na mtoto mdogo (amuachie mtu mwingine) – ni hatari kuwa katika vita ukiwa na watoto (ikibidi aje na msaidizi atakayekaa na mtoto huko nje). Mtoto anaweza kuathirika kisaikolojia anapoona mapepo yanavyomtesa mzazi wake. Lakini pia huduma haitafanyika katika utulivu kama kuna watoto wadogo.
5. Mhitaji avae nguo za kujisitiri ili kama ana mapepo yasimdhalilishe – Tunapendekeza kama ni mwanamke avae gauni refu ambalo halijambana badala ya sketi na blauzi. Mwanaume pia avae suruali ambayo haijambana sana.
6. Mhitaji ajiandae maji yake ya kunywa na kujihudumia kwa chakula na mahitaji mengine binafsi. Kuna nyumba za wageni na mgahawa karibu na kanisa. - Huduma hii inatolewa bure na hatuuzi vifaa vyovyote kv maji, mafuta na vitambaa. Bwana aliyetupa huduma hii ametuonya tusiwatoze watu tunapowahudumia. Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”
7. Kuna wakati huduma hii inafanyika kwa njia ya mtandao (kukitokea dharura) kv Whatsapp meeting calls, Zoom, Google meet nk.
Ratiba inaweza kubadilika kutokana na dharura za huduma zingine au safari. Hivyo wasiliana na wahudumu wakujulishe kama kuna mabadiliko yoyote.
Tuko Korogwe mjini karibu na Magereza kando ya barabara ya Maembe kwenda NSSF. Utaona kanisa la Transformed Life Mission Church (TLMC).
KWA WANAOTAKA KUSHIRIKI KWA NJIA YA MTANDAO
Unaweza kushiriki vipindi kwa njia ya mtandao au kupewa appointment ya kuombewa kwa njia ya mtandao.
Kwa mwenye Whatsapp unaweza kunijulisha majina yako, ulipo, mahitaji yako, maelezo machache ya hatua ulizowahi kuchukua na matokeo uliyopata, muda na siku ambazo unaweza kushiriki nk.
Hakikisha ume-save namba yangu ya simu na whatsap yako ina picha yako ndipo itakuwa rahisi kukutumia kiungo (link) ili ushiriki. Usisahau kujiunga kifurushi cha mtandao wa simu ambao una nguvu hapo ulipo ili mawasiliano yasikatikekatike. Tutatumia zaidi ‘audio’ badala ya ‘video’ ili hata wenye mtandao dhaifu waweze kushiriki. Kumbuka kuzima mic (mute) hadi pale unapopewa nafasi ya kuongea. Itasaidia kelele za mahali ulipo zisiathiri huduma inayoendelea mtandaoni.
Kumbuka: Atakayepokea ujumbe wa kushiriki huduma
ya mtandaoni kwa whatsap ni yule tu aliye-save namba yangu kwenye simu yake. Lakini
pia kuna ukomo wa idadi maalum ya washiriki.
Kama watakuwepo washiriki wasiojua Kiswahili, tutachanganya na lugha ya Kingereza ili nao wasiachwe kabisa.
Unaweza kupata maelekezo zaidi kupitia kupitia tovuti ya www.lawimshana.com (Faith and Community Empowerment). Nenda kwenye “Google search” uandike Lawi Mshana, utaipata hii tovuti. Pia ndani ya Tovuti utaona DOWNLOAD APP ambapo utapata App ya ‘Faith Empower’ ili kupata huduma zote sehemu moja (all-in-one platform).
Kwa unayetaka kushiriki kipindi hiki kituoni, wasiliana nasi kupitia simu hizi: 0657-705509; 0775-591345; 0693-925055
Kwa huduma ya Kliniki ya Uponyaji mtandaoni wasiliana nami kwa Whatsapp kupitia 0688-986882.
Dr. Lawi Mshana, Tanzania