17. Benefit
from your anointing
(Upako ulio nao utumie kwako mwenyewe pia)
A person can have one type of anointing and not have another.
God allowed it that way so we can work together as a team. You fail to achieve
some things because you don't have their keys. We must function as members of
the Body of Christ. If you are a hand, don't force yourself to do assignments
of other organs. Don't walk acrobatically using your hands, you won't get far.
Instead, use your legs to bring you where you want so you can pick up your
item.
A person can also have the anointing but fail to use it. For example, a person can only use his anointing to rebuke demons and fail to use it to overcome the spirit of poverty. When the demons manifest, he rebukes them with great severity, but at home, he has serious problems. He has never prayed seriously for his house or rebuked the spirit of poverty tormenting him and he is not even ashamed. He sees it as normal to live in poverty. Even though God has given you the ministry of deliverance, don't just rebuke the demons that torment other people. Cast out also the demons that hold your blessings.
My testimony: God once gave me a revelation that there are demons that do not touch me but have blocked my ways of success. When I realized that and pulled down those strongholds, I received a financial breakthrough. 2 Corinthians 10:4 "(for the weapons of our war are not of the flesh, but have power in God to bring down fortresses;)" Therefore, it is important that we evaluate our lives and not justify our poverty.
2 Cor 10:4 “For the weapons of our warfare are not carnal but mighty in God for pulling down strongholds.”
Please send your love gift to support this ministry. +255 712924234 or CRDB Bank; Account Name: Lawi E. Mshana; Account Number: 0152219784300; Swift Code: CORUTZTZ
Mtu anaweza kuwa na upako wa aina fulani na asiwe na upako wa aina nyingine. Mungu amefanya hivyo ili tufanye kazi kwa ushirikiano. Kuna mambo hufanikiwi kwa vile huna funguo zake. Lazima tufanye kazi kama viungo katika mwili wa Kristo. Kama wewe ni mkono usilazimishe kwamba unaweza kufanya kazi za viungo vingine. Usitembee kwa sarakasi hutafika mbali. Badala yake mwambie mguu akusaidie ili ufike pale na kuweza kuokota.
Lakini pia mtu anaweza kuwa na upako lakini hautumii. Kwa mfano, mtu anaweza kuutumia upako wake kukemea mapepo tu na kushindwa kuutumia kushinda roho ya umasikini. Mapepo yanapojidhihirisha anayakemea kwa uzito mkubwa lakini nyumbani kwake ana matatizo makubwa. Hajawahi kuiombea nyumba yake kwa uzito wala kukemea roho ya umasikini katika maisha yake na wala hahukumiwi. Anaona ni kawaida tu kuishi katika umasikini. Pamoja na kwamba tumepewa huduma hiyo, usikemee tu mapepo yanayotesa watu wengine. Kemea pia mapepo yaliyoshikilia baraka zako.
Ushuhuda wangu: Mungu aliwahi kunipa ufunuo kwamba kuna mapepo hayanigusi mimi lakini yameshika njia zangu za mafanikio. Nilipotambua hilo na kuangusha hizo ngome ndipo nikaona upenyo katika maisha yangu. 2 Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)” Kwa hiyo ni muhimu tutathmini maisha yetu na wala tusitetee umasikini wetu.
Bofya video usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator
& Public Speaker, +255712924234, Tanzania