16. Know your anointing and use it well
(Tambua upako wako na kuutumia vizuri)
Seek the anointing of the Holy Spirit and use it. You may be filled with the power of the Holy Spirit but you don't know about the anointing of the Holy Spirit. A Christian may lack the anointing of the Holy Spirit or have the anointing and fail to use it. For example, if a traffic police in uniform does not stand on the road and stop the car, it will not stop by itself. Even if you are registered in the government of God and given authority if you do not use the authority given to you, many things will remain as they are because you do not take action. Heb 1:9 “You have loved righteousness and hated lawlessness; Therefore God, Your God, has anointed You With the oil of gladness more than Your companions."” There are different types of anointing. With this anointing of joy, you have the pleasure of serving God, even if others do not want to serve Him, you do not get tired, you are ready to pay for something by yourself if you have that ability, even if others do not give anything. You won't count how many people are in the church so everyone contributes. You realize that you are the keys to your church.
Please send your love gift to support this ministry. +255 712924234 or CRDB Bank; Account Name: Lawi E. Mshana; Account Number: 0152219784300; Swift Code: CORUTZTZ
Tafuta upako wa Roho Mtakatifu na kuutumia. Unaweza kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu lakini hujui kuhusu upako wa Roho Mtakatifu. Mkristo anaweza kukosa upako wa Roho Mtakatifu au awe na upako huo na kushindwa kuutumia. Mfano, kama askari polisi wa usalama barabarani atakuwa amevaa sare yake lakini hatasimama barabarani na kusimamisha gari, halitasimama lenyewe. Hata kama umesajiliwa kwenye serikali ya Mungu na kupewa mamlaka kama hutaitumia mamlaka hiyo uliyopewa, vitu vingi vitabaki kama vilivyo kwa sababu huchukui hatua. Ebr 1:9 “Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.” Kuna aina mbalimbali za upako. Ukiwa na huu upako wa shangwe unakuwa na raha ya kumtumikia Mungu, hata kama wengine hawataki kutumika wewe huchoki, uko tayari ugharamie kitu peke yako kama una uwezo huo hata kama wengine hawatoi chochote. Hutapenda kuhesabu mko wangapi kanisani ili kila mtu achangie. Unajitambua kwamba wewe ni funguo katika kanisa lako.
Bofya video usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.
Dr.
Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234,
Tanzania