Video link: Kanuni za mafanikio endelevu
PRINCIPLES OF SUSTAINABLE SUCCESS (KANUNI ZA MAFANIKIO ENDELEVU)
1. Hard work – A hardworking person has a greater chance of being promoted than a lazy person who does not like to put in the effort.
2. Patience—A proverb says, ‘A patient man will eat ripe fruit’. A patient person does not give up when he does not get results quickly.
3. Sacrifice – For a person to be successful, he must sacrifice himself and be frugal. Frugality has both a negative and a positive side. The negative side is being selfish and not caring about others. The positive side is not accepting spending your money without a clear plan.
4. Consistency – Learn to maintain the pace and standard of your performance for a long time. Do not change your plans without a reason.
5. Discipline – Learn to follow your schedule and have necessary expenses. Do not wait for someone else to push you to do your work.
6. Confidence – If you lack courage and bravery, you will give up so easily. Learn to overcome the fear of life and dare to take calculated risks.
KANUNI ZA MAFANIKIO ENDELEVU
1. Bidii ya kazi (hardwork) – Mtu mwenye bidii ya kazi anakuwa kwenye nafasi kubwa ya kupandishwa cheo kuliko mtu mvivu ambaye hapendi kujituma.
2. Uvumilivu (patience) – Kuna methali inayosema kwamba ‘mvumilivu hula mbivu’. Mtu mvumilivu hakati tamaa anapoona hapati matokeo kwa haraka.
3. Kujikana (sacrifice) – Ili mtu afanikiwe anatakiwa kujinyima na kuwa bahili (frugal). Ubahili una upande hasi na chanya. Upande hasi ni kuwa mbinafsi kiasi cha kutojali wengine. Upande chanya ni kutokubali kutumia pesa zako bila mpango unaoeleweka.
4. Uendelevu (consistence) – Unatakiwa kuendelea na kasi hiyo na viwango hivyo kwa muda mrefu. Usibadilike badilike.
5. Nidhamu (discipline) – Jifunze kufuata ratiba yako na kuwa na matumizi ya lazima. Usisubiri mtu mwingine akusukume kufanya kazi yako.
6. Ujasiri (confidence) – Ukikosa uhodari na ushujaa katika shughuli zako utakata tamaa haraka. Jifunze kushinda hofu ya maisha na kuthubutu kufanya mambo uliyoyafanyia tathmini (calculated risks).
Dr. Lawi Mshana, Workshop Facilitator, +255712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)