Ticker

6/recent/ticker-posts

A MARRIAGE WITHOUT LOVE LANGUAGES WILL BREAK UP (NDOA BILA LUGHA ZA UPENDO ITAVUNJIKA)

 

Video link: NDOA BILA LUGHA ZA UPENDO ITAVUNJIKA

A MARRIAGE WITHOUT LOVE LANGUAGES WILL BREAK UP

(NDOA BILA LUGHA ZA UPENDO ITAVUNJIKA)

When I say marriages will fall apart, I don't just mean couples separating or divorcing. I also suggest that people living together without true love, to the extent that they tolerate each other, or live only to raise their children.

All of these love languages ​​are important, but there is one that touches the heart of a couple the most, and that language does not necessarily suit everyone. What is required is to learn your partner's language and invest in it.

1. Words of affirmation

A person whose language is this is very touched by words such as sorry, thank you, and I love you. 

2. Quality time

A person whose language is this gives attention when they discuss, such as turning off the phone for a moment and listening to them.

3. Gifts

A person whose language is this is touched by gifts that speak to their heart. These gifts are more than the daily responsibilities of cooking or paying children's school fees.

4. Acts of service

A person whose language is this is deeply touched when they are warmly welcomed after a trip or work, or when they are accompanied to a place.

5. Physical touch

A speaker of this language is deeply touched when they are greeted or hugged by their partner. 

No language is suitable for everyone at all times (one-size-fits-all). Therefore, it is good to find time to discuss together instead of guessing.

Now you can contact me directly through the WhatsApp link on my website. The first link is more suitable for those who use smartphones, and the second link is for those who use computers.

Don't hesitate to reach out when you have a question, need advice, or have a testimony. 

NDOA BILA LUGHA ZA UPENDO ITAVUNJIKA

Ninaposema ndoa itavunjika sina maana tu ya wanandoa kutengana au kutalakiana. Nina maana pia ya watu kuishi pamoja bila mapenzi ya dhati kiasi kwamba wanavumiliana tu au wanaishi tu kwa ajili ya kulea watoto wao.

Lugha hizi za upendo zote ni muhimu lakini ipo moja ambayo inagusa zaidi moyo wa mwanandoa na sio lazima lugha hiyo imfae kila mmoja. Kinachotakiwa na kujifunza lugha ya mwenzako na kuwekeza hapo.

1. Maneno ya kuthibitisha

Mtu ambaye hii ni lugha yake, anaguswa sana na maneno kama vile pole, samahani, asante, na nakupenda.

2. Muda wa thamani

Mtu mwenye hii lugha anapenda sana mwenzake ampe usikivu anapohitaji kuongea naye kama vile kuzima simu kwa muda na kumsikiliza.

3. Zawadi

Mwenye lugha hii anaguswa na zawadi zinazozungumza na moyo wake. Zawadi hizi ni tofauti na majukumu ya kila siku ya kupika au kulipa ada za watoto shuleni.

4. Matendo ya huduma

Mwenye lugha hii anaguswa sana moyoni anapopokelewa akitoka safari au kazini au anaposindikizwa mahali.

5. Mguso wa kimwili

Mwenye lugha hii anaguswa sana mwenzake anapomuwao au kumkumbatia.

Hakuna lugha inayofaa kila mtu kwa kila wakati (one-size-fits-all). Kwa hiyo ni vizuri kupata muda wa kujadiliana ili msibahatishe.

Kwa sasa kuna kiungo (link) cha WhatsApp kwenye hii tovuti yangu ambapo unaweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja. Link ya kwanza inawafaa zaidi wanaotumia simujanja na link ya pili inafaa zaidi kwa wanaotumia kompyuta.

Jisikie huru kuwasiliana nami kama una swali, unahitaji ushauri au una ushuhuda kutokana na masomo unayoyapata hapa.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator & Mentor, +255712924234, Tanzania

Post a Comment

0 Comments