Ticker

6/recent/ticker-posts

Welcome to the Healing Clinic in towns and villages (Karibu Kliniki ya Uponyaji mijini na vijijini)


 Video link: Karibu Kliniki ya Uponyaji mijini na vijijini

Welcome to the Healing Clinic in towns and villages

(Karibu Kliniki ya Uponyaji mijini na vijijini)

We do this ministry every evening from 05.30 pm to 7 pm. This counseling and intercession service is provided free of charge. Sometimes we visit cities and villages to deliver this service to people. Some people need to be prayed for more than once. Even when the blind person was brought to Jesus, the healing was gradual and not instant. He chose to do it in a process. We want to know the source of the problem so that, in addition to praying for healing, we can also caution and warn you. We pray and monitor the changes that occur and advise them further. 

We welcome anyone who wants to donate to support this ministry. However, we do not allow anyone to pay for this ministry because it was freely given to us. Matthew 10:8 “Heal the sick, raise the dead, cleanse the lepers, cast out demons; freely you have received, freely give.”

In addition to this ministry, we provide community-based services and empower faith leaders from different denominations in the areas we reach. We raise our own funds to avoid burdening our hosts, many of whom have economic challenges.

This ministry has no religious discrimination. We know that the Lord Jesus did not bring religion to this world, but the Kingdom of God.

But we also strive to equip our clients to be ministers who can pray for themselves and intercede for others.

Karibu Kliniki ya Uponyaji mijini na vijijini

Tunafanya huduma hii kila siku jioni kuanzia saa 11.30 hadi saa 1 kasoro usiku. Huduma hii ya ushauri na maombezi inatolewa bure bila malipo yoyote. Kuna wakati tunatembelea miji na vijiji kwa ajili ya kufikisha huduma hii mahali watu walipo. Kuna watu wenye matatizo ambayo yanahitaji kuombewa zaidi ya mara moja. Hata Bwana Yesu alipoletewa kipofu amponye alimponya kwa mchakato na sio papo kwa papo. Tunapenda kujua chanzo cha tatizo ili pamoja na kukuombea uponyaji tuweze kukutahadharisha pia. Tunapenda kumuombea mtu kwa muda wakati tukifuatilia mabadiliko yanayotokea na kumshauri zaidi.

Hata hivyo tunashirikisha yeyote anayependa kutoa sadaka ya kutegemeza huduma hii lakini hatupendi mhitaji yeyote ailipie kwa vile tumepewa bure. Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”

Huduma hii inaambatana na huduma za jamii na kuwafikia watumishi wa Mungu kutoka madhehebu tofauti wa maeneo tunayofikia. Tunapenda kujitegemea bila kuwalemea wenyeji wetu ambao wengi wao wana changamoto nyingi za kiuchumi.

Huduma hii haina ubaguzi wowote wa kidini. Tunatambua Bwana Yesu hakuleta dini hapa duniani bali alileta ufalme wa Mungu.

Lakini pia tunapenda watu wanaoponywa kupitia huduma hii waandaliwe kuwa watumishi wanaoweza kujiombea na kuwaombea wengine.

Dr. Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania