Ticker

6/recent/ticker-posts

20th Wedding Anniversary of Pastor Ndwela and His Wife, Blandina


Video link: Maadhimisho ya miaka 20 ya ndoa ya mchungaji Ndwela na mkewe, Blandina

 20th Wedding Anniversary of Pastor Ndwela and His Wife, Blandina

We need to know the importance of remembering the events of victory in our lives. Joshua 4:5-7 “5 And Joshua said to them, “Go on ahead of the ark of the Lord your God into the middle of the Jordan, and take up each of you a stone on his shoulder, according to the number of the tribes of the children of Israel; 6 that this may be a sign among you, when your children ask you in time to come, saying, ‘What do these stones mean?’ 7 Then you shall say to them, ‘Because the waters of the Jordan were cut off before the ark of the covenant of the Lord; when it crossed over the Jordan, the waters of the Jordan were cut off; and these stones shall be a memorial to the children of Israel forever.”

Jer 6:16 “Stand in the highways, and see, and ask for the old paths, Where is the good way? Walk in it, and ye shall find rest unto your souls.”

The difference between Christian marriage and other marriages

In society, marriage is a contract between two people united by men (government, custom, leader), which can be broken at any time. 1+1=2

In Christianity, marriage is a covenant between two people united by God, so only God can break it. 1+1=1

Maadhimisho ya miaka 20 ya ndoa ya mchungaji Ndwela na mkewe, Blandina

Tunatakiwa kujua umuhimu wa kukumbuka matukio ya ushindi katika maisha yetu. Yoshua 4:5-7 “5 naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; 6 ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? 7 Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.”

Yer 6:16 “Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu.”

Tofauti ya ndoa ya Kikristo na ndoa zingine

Katika jamii, ndoa ni mkataba kati ya watu wawili waliounganishwa na wanadamu (serikali, mila, kiongozi) ambao unaweza kuvunjika wakati wowote. 1+1=2

Katika Ukristo, ndoa ni agano kati ya watu wawili waliounganishwa na Mungu hivyo ni Mungu tu anayeweza kuivunja. 1+1=1

Dr. Lawi Mshana, 0712-924234, Tanzania