A short clip from the first session (National Conference, KMMT Church, Handeni)
Youth Session:
A pastor's wife once testified that she wanted to marry a pastor who didn't have a fat belly. It so happened that when the Bible college students visited their church, she thought one of them would propose to her, but no one did. Later, she got engaged to someone who wasn't a pastor and had a fat belly. She strongly objected to it, but later she agreed. When she got married, God called her husband, and he became a pastor. After becoming a pastor, he went through many trials until his fat belly was gone. God doesn't necessarily answer your prayers before you get married. You can find some answers ahead in your life's journey.
The Entire Church Session
God performs miracles for necessary reasons and not for show. Jesus did not walk on water for show. It was required because the boat was in a stormy sea while he was on shore.
God gave the Israelites manna in the wilderness because they had no other way to get food while traveling in the wilderness. When they reached Canaan and were able to plant crops, God stopped the manna.
Kipande kifupi cha kipindi cha kwanza (Kongamano la Kitaifa, KMMT, Handeni)
Kipindi cha vijana:
Mama mchungaji aliwahi kutoa ushuhuda kwamba alitamani kuolewa na mchungaji ambaye hana kitambi. Ikawa kila wanafunzi wa chuo cha Biblia walipotembelea kanisa lao alidhani mmoja wao atamchumbia na hakuna aliyemchumbia. Baadaye akachumbiwa na mtu ambaye sio mchungaji na ana kitambi kikubwa. Alipinga sana jambo hilo ila baadaye akakubali. Alipoolewa, Mungu akamuita huyo mumewe na akawa mchungaji. Baada ya kuwa mchungaji akapita katika mapito mpaka kitambi kikaisha. Sio lazima Mungu akujibu maombi yako kabla ya ndoa. Majibu mengine unaweza kuyapata mbele ya safari ya maisha.
Kipindi cha Kanisa Zima
Mungu anatenda miujiza kwa sababu za lazima na sio kwa ajili ya maonyesho. Yesu hakutembea juu ya maji kwa ajili ya maonyesho. Kulikuwa na ulazima kwa vile mashua ilikuwa na msukosuko katikati ya bahari wakati yeye akiwa pwani.
Aliwapa Wana Waisraeli mana jangwani kwa vile hawakuwa na namna nyingine ya kupata chakula wakiwa safarini jangwani. Walipofika Kanaani na kuweza kupanda mazao, Mungu alikomesha mana.
Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania