Ticker

6/recent/ticker-posts

Thanks to the churches and community of Ntenga, Same

Video link: Thanks to the churches and community of Ntenga, Same

Thanks to the churches and community of Ntenga, Same

I would like to take this opportunity to thank God for the way He has enabled us in the ministry we did in the Upareni mountains in Ntenga village, Same district, in Kilimanjaro region. We saw God working in a very special way in the ministry that was held for eight days. We are very grateful to the servants of God from various denominations who responded to the call and were willing to participate with their members to learn the word of God together. We did not lack, as people gave us food and cooperated with us, and thus God was exalted and glorified. We saw extraordinary hospitality from the people of Ntenga and neighboring villages. I also had the opportunity to visit the elderly neighbors who supported our parents in raising us. When God gives me the privilege, I also reach out to the elderly.

I would like to express my gratitude to the Ntenga village government for making it possible for us to reach out to people from every neighborhood to provide them with training on gender-based violence and offer them a small fare and a gift of clothes that we get through our ministry partners. 

I also thank you for your prayers and support. I thank all those who gave their time and stopped their financial activities to accompany me in this ministry. We thank our neighbor, who is a Muslim, for offering his house to accommodate some of our team members. God will remember him for the service he did. 

I invite you to join us in this missionary work next time.

Shukrani kwa makanisa na jamii ya Ntenga, Same

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa namna ambavyo ametuwezesha katika huduma tuliyokuwa tukiifanya katika milima ya Upareni katika kijiji cha Ntenga, wilaya ya Same, mkoa wa Kilimanjaro. Tulimuona Mungu akitenda kazi kipekee sana katika huduma ile ambayo ilifanyika kwa siku nane. Tunashukuru sana kwa ajili ya watumishi wa Mungu kutoka madhehebu mbalimbali ambao waliitikia wito na kuwa tayari kushiriki pamoja na washirika wao ili kujifunza pamoja neno la Mungu. Hatukupungukiwa kwa vile watu walijitoa sana kutupa vyakula na kushirikiana nasi na hivyo Mungu akainuliwa na kutukuzwa. Tuliona ukarimu wa kipekee kutoka kwa watu wa Ntenga na vijiji jirani. Pia nilipata nafasi ya kuwatembelea wazee majirani ambao walishirikiana na wazazi wetu kutulea. Mungu anaponipa nafasi ninawafikia pia wazee.

Napenda kutoa shukurani zangu kwa serikali ya kijiji cha Ntenga. kwa jinsi ambavyo walituwezesha kupata watu kutoka kila kitongoji kwa ajili ya kuwapa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia na kuwapatia nauli kidogo na zawadi ya nguo tunazopata kupitia kwa marafiki wa huduma yetu.

Nashukuru pia kwa ajili yako uliyetoombea na kuhusika kwa hali na mali. Nawashukuru wote waliotoa muda wao wakasimamisha kazi zao na kufuatana na mimi katika huduma hiyo. Tunamshukuru jirani yetu ambaye ni Muislamu kwa kutoa nyumba yake kwa ajili ya malazi ya baadhi ya watumishi wa huduma hii. Mungu atamkumbuka kwa ajili ya utumishi alioufanya.

Nakukaribisha wakati mwingine ushirikiane nasi katika huduma hii ya kimisheni.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania