Ticker

6/recent/ticker-posts

A short clip from the eighth day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)

Video link: Siku ya nane: Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi

A short clip from the eighth day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)

Judges 6:15 “And she said unto him, O Lord, how shall I save Israel? Behold, my family is the poorest in Manasseh, and I am the least in my father’s house.” Do not cling to your bad history. Even though God has called you, something is pulling you back to examine your weaknesses. God wanted to trust Gideon, but he did not consider himself worthy. Mary did well to accept the call to give birth to Jesus. Luke 1:38 “And Mary said, Behold, I am the handmaid of the Lord; let it be to me according to your word.” And the angel departed and went his way.” Zechariah said it was not easy and was struck dumb. Luke 1:20 “And behold! You will be mute, unable to speak, until the day these things take place, because you did not believe my words, which will be fulfilled in their season.” Lest you too be struck dumb because you do not want to understand God. God wants to send you to foreign lands, but you defend yourself by saying that you do not know English. We do not go by speaking English but by the anointing of the Holy Spirit. Even those who know English when they come to preach to us are helped by interpreters. Do not have excuses when God sends you.

Kipande kifupi cha siku ya nane

(Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi, Ntenga, Same)

Amu 6:15Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.Using’ang’anie historia yako mbaya. Ingawa Mungu amekuita, kuna kitu kinakuvuta nyuma ili uangalie udhaifu wako. Mungu alitaka kumtumaini Gideoni lakini yeye akajiona hafai. Mariamu alifanya vizuri kwa kuukubali wito wa kumzaa Yesu. Luka 1:38 “Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.” Zakaria alisema sio rahisi akapigwa ububu. Lk 1:20 Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.Isije ikawa hata wewe umepigwa ububu wa aina fulani kwa sababu hutaki kumuelewa Mungu. Mungu anataka kukutuma nchi za nje lakini unajitetea kwamba hujui Kingereza. Hatuendi kwa kuongea kingereza bali kwa upako wa Roho Mtakatifu. Hata wanaojua kingereza wanapokuja kutuhubiri wanasaidiwa na wakalimani. Usipende kuwa na udhuru pale Mungu anapokutuma.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania