Ticker

6/recent/ticker-posts

A short clip from the fifth day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)


 Video link: Siku ya 5: Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi

A short clip from the fifth day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)

Believing that prayer is the answer to everything is not entirely accurate. Some people believe that fasting and praying will bring them financial success. Usually, when you pray and fast, you draw closer to God and hear God more easily. You will not be given money easily, but you will hear God more easily. You will discover where God wants you to get money from or who has your blessings. Prayer will not cause you to pick up money on the road that others have sought and dropped. We also need to find quiet time in prayer and turn off the phone when we pray. PRAYER DOES NOT DO EVERYTHING, BUT PRAYER IS THE BEGINNING OF EVERYTHING. Not everything will be done by praying. But you will also not succeed in anything if you do not start with prayer. There are living examples in the Bible. God works with humans. For example, He did not save Cornelius himself but directed him to Peter to be preached to. But he also used Ananias (just a believer) to pray for Paul when he met Jesus on the road. We need the guidance of the Holy Spirit.

Kipande kifupi cha siku ya tano

(Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi, Ntenga, Same)

Kudhani maombi ni jibu la kila kitu sio sahihi. Kuna watu wanadhani kwamba kama watafunga na kuomba pesa zitakuja. Kwa kawaida unapoomba na kufunga, unasogea karibu na Mungu na kumsikia Mungu kwa wepesi. Hutapewa pesa kwa wepesi ila utamsikia Mungu kwa wepesi. Utagundua Mungu anataka ukapate pesa wapi au nani ana baraka zako. Maombi hayatasababisha uokote pesa njiani ambazo zimetafutwa na wengine wakaziangusha. Lakini pia tunatakiwa tupate muda wa utulivu katika maombi na kuzima simu tunapoomba. MAOMBI HAYAFANYI KILA KITU ILA MAOMBI NI MWANZO WA KILA KITU. Si kila jambo litafanyika kwa kuomba. Lakini pia hutafanikiwa katika jambo lolote kama hutaanza na maombi. Ipo mifano hai katika Biblia. Mungu anatenda kazi pamoja na wanadamu. Mfano, Hakumuokoa Kornelio yeye mwenyewe bali alimuelekeza kwa Petro akahubiriwe. Lakini pia alimtumia Anania (muumini tu) kumuombea Paulo alipokutana na Yesu akiwa njiani. Tunahitaji uongozi wa Roho Mtakatifu.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania