Ticker

6/recent/ticker-posts

A short clip from the fourth day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)

Video link: Siku ya 4: Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi

A short clip from the fourth day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)

We need to be blessed to the same extent that Jesus fed people. Even when we are able, we do not plan to organize a celebration and feed people. We have decided to organize celebrations according to biblical principles. The guests will not donate but will bring their gifts. Right now, a person pays more for the food they will eat at the party. We also want to invite the less fortunate so that we can be rewarded. Luke 14:13,14 “But when you give a banquet, invite the poor, the crippled, the lame, the blind, and you will be blessed, because they have nothing to repay you; for you will be repaid at the resurrection of the righteous.” Today's parties are only attended by those who donated. Those who are financially unable, even if they are the ones who prayed for the young man to find a life partner, do not qualify to enter the wedding hall. Therefore, we have agreed with our church to have a church party right after the wedding to bid farewell to the bride and groom. The groom's relatives will organize their party at the hall after that. This will also help us give them gifts that meet their needs. Some brides are forced to sell gifts so they can afford food. I know it will take time for people to understand, but they will understand eventually. It is not good to donate to the celebration more than our basic needs. If we do not pay attention, we will not make any progress in life. However, we will not stop their relatives from holding their celebration.

Kipande kifupi cha siku ya nne

(Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi, Ntenga, Same)

Tunatakiwa kubarikiwa kwa kiwango ambacho kinafanana na Yesu alivyowalisha watu. Hata tunapokuwa na uwezo hatuna mpango wa kuandaa sherehe na kuwalisha watu. Sisi tumeamua kuandaa sherehe kwa kufuata misingi ya kibiblia. Waalikwa hawatachangia bali watakuja na zawadi zao. Sasa hivi mtu analipia zaidi ya chakula atakachokula kwenye sherehe. Sisi tunataka kuwaalika pia watu wasiojiweza ili tupate thawabu. Luka 14:13,14 “Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.” Sherehe za leo wanaalikwa waliochangia tu. Wasio na uwezo wa kifedha hata kama ndio waliomuombea kijana akapata mwenzi wa maisha, wanakosa sifa za kuingia ukumbi wa harusi. Hivyo tumekubaliana kanisa letu kuwa na sherehe ya kanisani baada tu ya ndoa kufungwa ili tuwaage maharusi. Ndugu za mahuarusi wataendelea na sherehe yao ukumbini baada ya hapo. Hii itasaidia tuwape pia zawadi zinazoendana na mahitaji yao. Baadhi ya maharusi wanalazimika kuuza zawadi ili waweze kupata chakula. Najua itachukua muda watu kuelewa lakini wataelewa badae. Sio vizuri kuchangia sherehe kuliko mahitaji yetu ya msingi. Tusipoangalia hatutakuwa na maendeleo yoyote. Hata hivyo hatutawazuia ndugu za maharusi kufanya sherehe yao.

Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania