Video link: Siku ya tatu: Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi
A short clip from the third day (Spiritual and economic breakthrough seminar, Ntenga, Same)
I wish God would give us a bigger picture so that sometimes the churches we participated in this seminar can reach other areas. A selfish vision causes us to miss blessings because we do not fulfill the command to reach out to Samaria and the whole world. Acts 1:8 “But you will receive power when the Holy Spirit has come upon you; and you will be my witnesses in Jerusalem, and in all Judea and Samaria, and to the ends of the earth.” All these years, we have served in one area without even reaching out beyond our wards or counties. This seriously threatens our security. We need to reach out to other people, even if we don't have a branch of our church in their areas. If we do so, we will receive a great reward. I want you to know why, in front of the church, I have written, EMPOWERMENT AND RETREAT CENTER. It means that it is a place to build people's capacity and be used for solitude prayers. Even at Korogwe, I once offered a prayer room for a pastor who was opening a church. I did not see it as a threat simply because he was from another denomination. Even when I started a church, I received a preacher of the Gospel, and did not have enough space to accommodate him. So I asked the pastor of the ELCT church to provide us with rooms for the preacher and his team. Even in this seminar, a Muslim neighbor has hosted some of our team members. We are making God's work difficult for no reason.
Kipande kifupi cha siku ya tatu
(Semina ya upenyo wa kiroho na kiuchumi, Ntenga, Same)
Natamani Mungu atupe picha kubwa ili wakati mwingine makanisa tulioshiriki semina hii tuyafikie maeneo mengine. Maono ya kichoyo yanatufanya tukose baraka kwa vile hatutekelezi agizo la kufikia Samaria mpaka mwisho wa nchi. Matendo ya Mitume 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Miaka yote tunatumika eneo moja bila kutoka hata nje ya kata zetu. Hii ni hatari sana kwa usalama wetu. Tunatakiwa kuwafikia watu wa mbali hata kama hatuna tawi la kanisa letu huko. Tukifanya hivyo tutapata thawabu kubwa. Napenda mjue kwanini mbele ya kanisa nimeandika, EMPOWERMENT AND RETREAT CENTER. Ina maana kwamba ni mahali pa kujengea watu uwezo na kutumiwa kwa ajili ya maombi ya utulivu. Hata Korogwe nilipo nimewahi kutoa chumba kwa ajili ya mchungaji anayefungua kanisa ili apatumie kwa maombi. Sikumuona kwamba ni tishio kwangu kwa vile anatoka dhehebu jingine. Hata mimi wakati naanza kanisa nilimpokea mhubiri wa Injili nikakosa malazi kwa ajili yake. Hivyo nikamuomba mchungaji wa kanisa la KKKT akanipa vyumba kwa ajili ya mhubiri na timu yake. Hata katika semina hii jirani Muislamu amepokea baadhi ya wahudumu wetu. Ni sisi wenyewe tunaifanya kazi ya Mungu iwe ngumu bila sababu.
Dr. Lawi Mshana, Facilitator and Public Speaker, +255712924234, Tanzania