NA 2: KWANINI KAMA MTU WA MUNGU UNATAKIWA KUFANANA NA TAI
(NO 2: WHY, AS A MAN OF GOD, SHOULD YOU BE LIKE AN EAGLE)
2. TAI ANA MAONO MAKUBWA – Anaona umbali wa maili 3 kutoka juu hadi kwenye kitoweo (prey) ambacho kiko ndani ya maji au nchi kavu. Akishuka kwa kasi analenga palepale alipo samaki au mnyama na kumchukua. Hata wewe unatakiwa kuwa na maono makubwa. Uone maisha yako yatakavyokuwa miaka mitatu mbele badala ya kuona mwezi mmoja ujao. Usifanane na kuku ambaye anafugwa na anaona wenzake wakichinjwa lakini hakimbii. Unatakiwa kuona mwaka 2030 utakuwa nani. Vinginevyo pesa zako zote zitaishia kwenye sikukuu na kuanza kulalamika kwamba Januari ni ngumu kiuchumi. Januari sio ngumu ila wewe ndiye mgumu kuelewa na kusoma nyakati. Unatakiwa kuwa na shabaha kama tai anavyomlenga mnyama anayetaka kumchukua. Hutafanikiwa kwa kufanya maombi peke yake bali kwa kutambua unatakiwa uanzie wapi. Shida yetu kubwa sio pesa bali hatuna vipaumbele (scale of preference). Hata Mungu hakumuumba Adamu mpaka alipoumba vitu atakavyohitaji Adamu. Mungu atusaidie kuona mbali kama tai na kufanya vitu ambavyo vinatekelezeka.
NO 2: WHY, AS A MAN OF GOD, SHOULD YOU BE LIKE AN EAGLE
2. THE EAGLE HAS BIG VISION – It can see 3 miles from above to its prey that is in the water or on land. When it swoops down, it aims for the fish or animal and takes it. You, too, need to have a big vision. See what your life will be like three years ahead instead of seeing one month ahead. Don’t be like a chicken that is being raised and sees its fellows being slaughtered but doesn’t run away. You need to see who you will be in 2030. Otherwise, all your money will end up on holidays, and you will start complaining that January is economically difficult. January is not difficult, but you are the one who is difficult to understand and know the times. You need to have a target like an eagle aiming for the animal it wants to take. You will not succeed by praying alone but by realising where you need to start. Our biggest problem is not money; we simply lack a clear scale of preference. Even God did not create Adam until He created the things that Adam would need. May God help us to see far like an eagle and do feasible things.
Dr. Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania


