NA 7: KWANINI KAMA MTU WA MUNGU UNATAKIWA KUFANANA NA TAI
(NO 7: WHY, AS A MAN OF GOD, SHOULD YOU BE LIKE AN EAGLE)
7. TAI AKIZEEKA ANAJITESA KWA AJILI YA MAISHA MAPYA
Tai akiwa na miaka 30 hivi manyoya yanamfanya ashindwe kwenda kasi. Hivyo anaenda mafichoni kwa miezi mitano. Anagonga mdomo wake kwenye mwamba, anang’oa makucha yake na kisha manyoya yake na kusubiri yaote mengine mapya. Hakati tamaa ya kuishi.
Akifanya hivyo, anapata maisha mapya na kuweza kuishi kwa miaka mingine 30 au 40.
Hapa tunajifunza kwamba tunatakiwa kuacha tabia za zamani (kuacha ya kale) na kuwa na muda wa faragha na Mungu (mahali pasipokuwa na watu). Marko 6:31a “Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo.”
Jifunze kutesa na kuutumikisha mwili wako. 1 Wakorintho 9:27 “bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.”
7. WHEN AN EAGLE GETS OLD, IT PERSEVERES FOR A NEW LIFE
When an eagle is about 30 years old, its feathers make it unable to move fast. So it goes into hiding for five months. It hits its beak on a rock, plucks its talons and then its feathers, and waits for new ones. It does not give up on living.
By doing so, it gains a new life and can live for another 30 or 40 years. Here we learn that we need to put away old habits and have some time alone with God (a solitary place). Mark 6:31a “And he said to them, Come ye yourselves apart into a desert place, and rest a while.”
Learn to subdue and bring your body under control. 1 Corinthians 9:27 “But I subdue my body, and bring it into subjection: lest, when I have preached to others, I myself should be disqualified.”
Dr Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania


