Video link: Na 2. Jali wito wako au kazi yako
Godly Ways to Get Money for Ministry and Business No. 2: Take care of Your Calling or Work (Njia za ki-Mungu za kupata fedha za huduma na biashara Na 2: Jali wito wako au kazi yako)
Luke 10:9 “Heal the sick who are there, and tell them, ‘The Kingdom of God has come near to you.’” The Lord Jesus gave his disciples a work to do. He gave them a specific ministry to care for. Sometimes we see a shopkeeper caring more about chatting on his phone than about customers. Maybe it’s his brother’s shop, so even if he doesn’t sell, it won’t affect his home budget. When you work, you must have a goal. Whom do you want to be in the next two or three years? The Lord Jesus gave his disciples a specific message to preach. When you care about your calling, the angel of God protects you. We must see the growth of your calling and your work.
Njia za ki-Mungu za kupata fedha za huduma na biashara Na 2: Jali wito wako au kazi yako
Lk 10: 9 “waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.”. Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake kazi ya kufanya. Aliwapa kazi maalum ambayo walitakiwa kuijali. Unaweza kukuta muuzaji wa duka anajali ku-chat na simu yake kuliko wateja. Pengine ni duka la kaka yake ambalo hata asipouza atapewa tu chakula nyumbani. Kutokuuza hakuathiri bajeti yake nyumbani. Unapofanya kazi lazima uwe na shabaha. Unataka kuwa nani miaka miwili au mitatu ijayo. Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake ujumbe maalum wa kuhubiri. Unapojali wito wako malaika wa Mungu anakulinda. Lazima tuone ukuaji wa wito wako na kazi yako.
Dr Lawi Mshana, +255712924234, Tanzania


