We are very grateful to the Director of the Korogwe Town Council for providing us with land experts who yesterday offered valuable education and responded to various concerns and questions about land matters at the TLMC Manundukati Hall. We greatly benefited from learning about the different responsibilities of land offices, the procedures for buying and selling plots, ways to avoid debts when purchasing plots, and many other important issues.
We often blame the land and town-planning departments for problems that result from our own mistakes, such as taking shortcuts and failing to attend empowerment workshops.
I also sincerely thank the neighbors who participated despite our religious and denominational differences.
This meeting was organized by our NGO, Beyond Four Walls, whose mission is to empower communities to overcome vulnerability, poverty, and dependency through participatory development approaches.
TUMEELIMIKA KUHUSU UMILIKI NA MATUMIZI YA ARDHI ILI KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA
Tunamshukuru sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe kwa kutupatia wataalamu wa ardhi ambao walitoa elimu na kujibu kero na maswali mbalimbali kuhusu ardhi katika ukumbi wa TLMC Manundukati jana. Tulinufaika kwa kutambua mgawanyo wa majukumu idara yao (vitengo vyao), mchakato wa kununua na kuuza viwanja, kuepuka madeni katika kununua viwanja nk.
Mara nyingi tunailaumu idara ya ardhi na mipango miji kwa makosa yetu wenyewe ya kutafuta njia za mkato na kutokuwa tayari kupata elimu.
Nashukuru pia majirani ambao walishiriki bila kuangalia tofauti zetu za kidini na kimadhehebu.
Mkutano huu uliandaliwa na NGO yetu ya Beyond Four Walls ambayo dhima yake ni kujengea uwezo jamii ishinde, uhatarishi, umaskini na utegemezi kwa kutumia mbinu shirikishi za maendeleo.
Dr Lawi Mshana, Executive Director, +255712924234, Tanzania




