Ticker

6/recent/ticker-posts

Mlinde kijana mtandaoni

MLINDE KIJANA MTANDAONI Haitoshi kuwaambia vijana wawaepuke watu wasiowajua. Vijana wanahitaji mbinu za kuwasaidia kushinda vishawishi hivi hasa wanapokuwa mtandaoni. Changamoto tuliyo nayo wazazi na walezi ni kwamba watoto tunaowatahadharisha wanajua mitandao ya jamii kuliko sisi wenyewe. Kibaya zaidi hatutaki kujifunza mambo ya msingi kuhusu uzuri na uhatarishi wa kuwa mtandaoni. Kama wazazi na walezi tufanye nini: • Tuwakumbushe vijana wetu kwamba watu hawako hivyo wanavyosema wakati wote mtandaoni. Anaweza akadhani anawasiliana na msichana mwenzake kwa vile tu ameweka picha ya msichana na kumbe ni mwanaume mwenye nia mbaya na yeye. • Mueleze kwanini ni hatari kutoa taarifa zake binafsi kwa mtu asiyemjua kama vile majina yake kamili au mahali anapopatikana. Mtu anapojua taarifa za kina za mtu ni rahisi kudhaniwa kwamba ni ndugu yake hata anapouliza majirani wa kijana. • Hakikisha anajua jinsi ya kumzuia (block) mtu asiyemuhitaji au anayemsumbua anapokuwa mtandaoni na jinsi ya kumripoti kwenye huo mtandao wa jamii. Kumbuka hutaweza kumsaidia kijana kama wewe mwenyewe unalazimika kuona picha mbaya usizozihitaji unapokuwa mtandaoni na huwezi kufanya chochote. Wakati mwngine unashangaa tu simu yako ina picha za aibu kiasi kwamba hata watoto wako wanaweza kukushuku vibaya. Shirika letu la Beyond Four Walls kupitia programu yake ya kuwasaidia watoto na vijana (adolescents and youth) pamoja na wazazi/walezi wao tunalenga afya ya uzazi, teknolojia na kukuza kipato. Programu hiyo inaitwa NITATOBOA. Jisajili uweze kukaribishwa ujifunze kwa njia ya midahalo, warsha, darasa au mtandaoni.