Ticker

6/recent/ticker-posts

Uanafunzi (sehemu ya pili)

3. Mwanafunzi lazima:- a) Ajifunze kwa mwalimu wake (head knowledge). Ni muhimu mwanafunzi kuwa na mwalimu wa kumpa mafundisho ya kiroho badala ya kutegemea mafundisho ya kidini. b) Apende mafundisho (heart knowledge). Hapa anakubali kwamba haya mafundisho ni kwa ajili yake. Hatafuti kujifunza kwa ajili ya watu wengine. c) Atendee kazi (applied knowledge). Hapa mafundisho yanakuwa sehemu ya maisha yake. Anayatumia kuleta mabadiliko maishani mwake. d) Ashirikishe (transferred knowledge). Hapa anayashirikisha kwa wengine 2 Tim 2:2. Hapa ndipo anafikia hatua ya kuyashirikisha kwa wengine kwa vile yamembadilisha yeye mwenyewe tayari. 4. Petro, Barnaba na Paulo Petro hakuwa na elimu ya kidunia isipokuwa alijifunza kwa Yesu na akawahubiri maelfu wakaokoka. Mdo 2:40, 41 ‘Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu’. Ni Barnaba aliyemlea Paulo. Mdo 9:26-27 ‘Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu’. Walisafiri pamoja katika huduma (Mdo 11:25-26) mpaka walipopishana kwa ajili ya Yohana Marko aliyewaacha katika safari za kimisheni (Mdo 15:36-40). Barnaba alichagua kumchukua Yohana Marko kwa ajili ya kumfanyia uanafunzi zaidi. Baadaye akafaa zaidi hata kwa Paulo. Kol 4:10 ‘Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni’. Paulo alimfanyia uanafunzi Timotheo ili aiendeleze huduma pale aliposhindwa kuendelea mwenyewe. 1 Tim 1:2,3 ‘kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine’. 5.Wakristo waliokomaa wanafananaje? Efe 4:13 ‘ – hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo’. Hili ndilo lengo letu. Lakini kivitendo ina maana gani? a) Wako salama katika uhusiano wao na Kristo. 1 Yoh 5:11-13 Wanajua wana uzima wa milele. b) Wanatambua mamlaka ya Bwana Yesu maishani mwao. Kol 2:6-7; 1 Kor 8:6. c) Wana ushindi katika dhambi maishani mwao. 1 Yoh 5:4-5; 1 Kor 10-13. d) Wanayajua maandiko na wanaweza kuyatumia inavyotakiwa katika maisha yao. 2 Tim 3:16-17 e) Wana maisha ya maombi yenye matokeo. Fil 4:6-7; 1 The 5:16-18. f) Tunda la Roho linaonekana maishani mwao. Gal 5:22-23; Yn 15:8. g) Wana utii katika kumtumikia Bwana. Yn 14:15,23; 1 Yoh 2:3. h) Wanashirikisha kikamilifu imani yao kwa wengine. 1 Pet 3:15. i) Wanashiriki kikamilifu katika ushirika wa Kikristo (ibada). Ebr 10:24-25. j) Wana huruma ya Kristo kwa ajili ya wengine na wako tayari kuwasaidia wengine. Kol 3:12-14; 2 Kor 9:7; Efe 4: 11-14. Somo hili litaendelea…