Ticker

6/recent/ticker-posts

Sasa unaweza kujiunga na kundi letu la kukabiliana na uhatarishi na majanga


 MZUNGUKO WA USIMAMIZI WA MAJANGA (DISASTER MANAGEMENT CYCLE)

Phase 1: Mitigation (kupunguza madhara)

Maana: Kuzuia majanga kwa siku zijazo na kuchukua hatua za kupunguza madhara – kupunguza uhatarishi kv uharibifu wa mali, kujeruhiwa na kupoteza maisha
Mf. Kuimarisha jengo, kujua ardhi inavyofaa kutumiwa (zoning) nk

Phase 2: Preparedness (maandalizi ya kukabiliana)

Maana: Kuchukua hatua kabla ili kuwa tayari kwa ajili ya dharura

 

Mf. Kutoa mafunzo na elimu

Phase 3: Response (mwitikio wa dharura)

Maana: Kuwalinda watu na mali kunapotokea janga (mara tu baada ya janga kutokea)
Mf. Kutathmini uharibifu na kutoa msaada

Phase 4: Recovery (Ukarabati)

Maana: Kujenga tena baada ya janga ili kurudisha hali kama ilivyokuwa mwanzo
Mf. Kushughulikia madhara makubwa yaliyotokana na janga
 

Maelezo ya ziada

Niliona umuhimu wa kupata haya mafunzo kupitia shirika la kimataifa, kwa vile dhamira ya shirika letu la Beyond Four Walls ni KUJENGEA UWEZO JAMII ISHINDE UHATARISHI, UTEGEMEZI NA UMASIKINI KWA KUTUMIA MBINU SHIRIKISHI. Kwa kawaida jamii imezungukwa na raslimali nyingi lakini wengi wetu tunaanza kuwapatia pesa badala ya kuwasaidia kutambua raslimali walizo nazo na kuzitumia kwanza.

Tunamchangia pesa mtu ambaye amezungukwa na watu ambao wangeweza kumsaidia kama tungewashirikisha. Hata hivyo mtu anapopata dharura inaweza kutulazimu kumsaidia kwa haraka. Lakini tulipaswa kufanya tathmini ili kuona kama hiyo ndiyo njia sahihi ya kumsaidia. Mfano, tunaweza kumchangia bati mzee fulani ili akae kwenye nyumba salama lakini hatujafuatilia kiwanja kimeandikwa jina la nani. Inawezekana baada tu ya kujengewa nyumba akafukuzwa maana sio cha kwake. Lakini pia kama umri wake umesogea sana, tulipaswa kumpatanisha na watoto wake walioko Dar wamchukue wakamlee. Lazima tujihoji kwanini ana watoto wenye uwezo lakini wamemtelekeza.

Lakini pia nilijifunza namna ya kuzitumia taasisi za dini kwa vile zina watu wengi ambao wako tayari kujitolea na wenye ujuzi wa aina nyingi. Lakini pia taasisi za dini zina raslimali kwa ajili ya dharura mbalimbali. Hivyo tumeanza na kanisa la TLMC ambapo tumeunda kamati ya usimamizi wa majanga yenye wajumbe 9 wenye kazi tofauti tofauti. Mbeleni tutajengea uwezo makanisa na misikiti mingine pia kwa vile BFW ni mratibu tu wa kuwezesha haya yafanyike kupitia jamii.

Unaweza kujiunga na Group letu la Vulnerability & Disaster Management (Kukabiliana na uhatarishi na majanga) ambalo liko Whatsapp kwa kuomba uingizwe kupitia namba 0688986882 na jingine ambalo liko Facebook (unaweza kutumiwa link yake kwa Whatsapp).

Toa maoni yako au uliza swali hapa chini palipoandikwa ENTER A COMMENT