WASAMARIA WEMA WAMENUSURU MAISHA YA MAMA NA MTOTO
Baada ya kupata mafunzo ya kukabiliana na majanga na kisha kuunda
kamati ya usimamizi, tumeweza kuhusika kumnusuru mama aliyepata uchungu akiwa
katika mazingira magumu. Alipata uchungu na akawa hana nauli hata ya bajaji
wala msaidizi yeyote nyumbani kwake. Tuliwapata wasamaria wengine walioungana
nasi kutoa mahitaji mbalimbali kama vile nauli ya kumkimbiza hospitalini, ndoo,
nguo za mama na za mtoto mchanga, chandarua cha mtoto na nauli za kumpeleka
kijijini kwa wazazi wake ili akapate uangalizi wa karibu baada ya kujifungua
salama. Wapo majirani waliokubali kuchukuliwa ghafla wakiwa njiani ili
wamsindikize hospitalini. Hata hivyo kwa mujibu wa kitengo chetu kazi bado haijaisha.
Anahitaji elimu zaidi atakaporudi ili kupunguza uwezekano wa tatizo hili
kujitokeza katika hali ya uhatarishi kiasi hicho.
Unaweza kuungana nasi kama Msamaria mwema wa kusaidia watu
wanapopata majanga, kusaidia kupunguza uwezekano wa majanga kutokea, kusaidia
kuponya kiroho na kihisia watu waliopata majanga nk.
Bilashaka unazo nguo na vitu mbalimbali ambavyo viko
nyumbani kwako kwa sasa na huvitumii kwa vile Mungu amekusaidia kupanda hatua
nyingine ya maisha. Pamoja na kwamba unayo pia mahitaji mengine, naomba Mungu
akupe moyo wa kutupatia vitu hivyo ili tuweze kutoa misaada ya dharura majanga
yanapotokea. Tutakutambua kama mshirika (partner) au ambassador (balozi) wa kushirikiana
na Beyond Four Walls katika kushughulika na uhatarishi na majanga yanayotokea
katika jamii.
Pia unaweza kujiunga na group letu jipya la Vulnerability
& Disaster Management (USIMAMIZI WA UHATARISHI NA MAJANGA) ambalo liko
Facebook na Whatsapp.
ANGALIZO: Beyond Four Walls sio shirika la kutoa misaada
bali kuhamasisha na kujengea uwezo jamii katika kukabiliana na uhatarishi na
majanga kwa kutumia mbinu shirikishi. Kwa ushirikiano wako tutaifikia jamii
nzima ya Kitanzania hatua kwa hatua.
Lawi Mshana, 0712-924234