Ticker

6/recent/ticker-posts

KIKAO CHA VIONGOZI WA DINI DODOMA KWA AJILI YA TATHMINI YA AWALI



 KIKAO CHA VIONGOZI WA DINI DODOMA KWA AJILI YA TATHMINI YA AWALI

Baada ya kukutana na viongozi wa serikali wiki zilizopita, leo tumekutana na viongozi wa dini kutoka madhehebu tofauti tofauti 16 ya Wakristo na Waislamu hapa jijini Dodoma. Lengo ni kupata ushirikiano wao katika zoezi hili la tathmini ya awali (needs assessment) ambalo limekaribia kufanyika rasmi. Zoezi hili litasaidia shirika letu la Beyond Four Walls lifanye maamuzi sahihi na kuungwa mkono na wadau katika shughuli za maendeleo ya jamii bila ubaguzi wa aina yoyote.

Tunashukuru viongozi wa serikali ambao walikuwepo kutufungulia kikao chetu.

Dr Lawi Mshana, Mkurugenzi Mtendaji, Beyond Four Walls.