Mungu anataka unufaike na taabu ya kazi zako
MUNGU
ANATAKA UNUFAIKE NA TAABU YA KAZI ZAKO
Watu wengi wanakumbuka tu kuomba wapate kazi au biashara na miradi yao ikue. Wanasahau kwamba mtu anaweza kuwa na kazi au ajira nzuri na miradi mizuri lakini hanufaiki nayo au haifurahii.
Zab 128:2 “Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.” (When you eat the labor of your hands, You shall be happy, and it shall be well with you). Mungu hataki ufanikiwe kwa kuchukua haki za watu wengine au kuwa mvivu. Lakini pia Mungu hataki watu wachezee haki zako alizokupa.
Mhu 5:18,19 “Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu; maana hilo ndilo fungu lake. Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.” (the gift of possessions and the power to enjoy them is a gift of God).
Unaweza kuonekana kwa nje kama unayefurahia maisha lakini kiuhalisia umekalia mwiba.
Kum 28:30-34 “30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake. 31 Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa. 32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako. 33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima; 34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona.”
Moja ya laana ni kutomfurahia mkeo au mumeo. Anakuwa tu ni baba watoto au mama watoto! Unaishi tu kwa ajili ya watoto wako.
Mit 3:1-10 “1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. 2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. 3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. 4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. 7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. 8 Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. 9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. 10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.”
Hata kama tunatafuta pesa tujue kwamba inatakiwa pesa ikutumikie na sio wewe kuitumikia.
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba ninufaike na taabu ya kazi za mikono
yangu nisiishi kama msukule unaowanufaisha wengine.
2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kufuata kanuni zako za
mafanikio ili nisiishi kwa taabu zisizo na matokeo chanya.
1 Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”
Dr. Lawi Mshana, +255712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao)

