WENYE HAKI ZAKO WATAKUTAFUTA (Video link)
WENYE
HAKI ZAKO WATAKUTAFUTA
Maono: Nimeona mtu akitafutwa ili akabidhiwe nyumba na mtu aliyekuwa ameandikishana mkataba na marehemu baba yake. Ingawa hakujua kama kulikuwa na mkataba wa aina hiyo.
1. Wenye mamlaka juu yako watakutendea haki
Mungu anataka kukupa kibali kwa wakuu wako ili wasikuonee tena bali wakupe haki zako bila masharti.
Isaya 60:17 “Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala; ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitawafanya wasimamizi wako wawe amani, Na hao wakutozao fedha kuwa haki.” (I will also make your officers peace, And your magistrates righteousness.)
2. Mitego uliyowekewa, haitafanikiwa
Kuna watu wanafanya vikao kwa ajili ya kukuangusha. Wataanguka wao wenyewe kwa vile Mungu ni mtetezi wako.
Isaya 54:14 “Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia. 15 Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako. 16 Tazama, nimemwumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu. 17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.”
3. Wenye njama na wewe, wataathirika wao
Maadui walipofanya njama ya kumuua Danieli, Mungu alimtetea. Madhara yakawapata wao wenyewe na familia zao.
Danieli 6:24 “Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.”
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unipe kibali kwa wenye mamlaka na haki
zangu. Wanihurumie na kunitendea haki.
2. Maneno mabaya ninayosemwa nayafuta katika Jina la Yesu.
Mashambulizi yanayotumwa kwangu hayatafanikiwa katika Jina la Yesu.
3. Wenye njama na mimi, wajue kwamba Mungu ni Mtetezi
wangu.
Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao)