MWILI UNAWEZA KUZUIA MAENDELEO YAKO (Bofya hapa uangalie video)
MWILI
UNAWEZA KUZUIA MAENDELEO YAKO (Soma
maandishi na kuangalia video fupi)
Kimsingi tuna maadui wakuu watatu. Maadui hao ni shetani, mwili na dunia. Kuna mambo mengi ambayo tunamsingizia shetani lakini kusema kweli sio yeye aliyasababisha. Mfano, mtu anapozini anaweza kumlaumu sana shetani lakini hakuna mtu amewahi kujikuta amevuliwa nguo na shetani. Anavua kwa uamuzi wake mwenyewe.
Rum 7:15-24 (viashiria kwamba una shida katika mwili wako)
1. Unatenda mambo unayoyachukia
Mst 15,19 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
2. Ndani yako halikai neno jema – umejaa taarifa mbaya tu
Mst 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
3. Unampenda Mungu ‘rohoni’ lakini viungo vya mwili vinakutuma kufanya mambo tofauti kabisa
Mst 22,23,24 - 22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, 23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. 24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
Ufanyeje?
1. Tambua
kwamba mwili ni adui
Warumi 8:7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni
uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
2.
Usulubishe mwili wako
Wagalatia 5:24 Na hao walio wa Kristo
Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
3. Enenda
kwa Roho
Wagalatia 5:16,17 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Mwaka 1996 Roho Mtakatifu alinipa dalili 20 za vifungo vya kiroho nikaandika jarida lenye kichwa UNAHITAJI HUDUMA MAALUM YA KUFUNGULIWA. Natarajia ujumbe huo upatikane kwa video hivi karibuni.
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unipe uwezo na nia ya kuudhibiti mwili
wangu ili niyafanye mapenzi yako.
2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuenenda kwa Roho ili
nisitimize kamwe tamaa za mwili.
Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao). Pia unaweza kuingia kwa urahisi katika majukwaa ya huduma hii yaliyoko
Facebook, Tiktok, Youtube, Soundcloud, Whatsap na Blog ukidownload na kuinstall
App ya LAWI MSHANA kupitia link hii LAWI MSHANA APP