FAHAMU MAPENZI YA MUNGU KWAKO (Bofya hapa uangalie video)
FAHAMU
MAPENZI YA MUNGU KWAKO
Kila mmoja wetu amewekwa hapa duniani kwa kusudi maalum.
Ndiyo maana alama za vidole gumba hazifanani. Hivyo si mpango wa Mungu uwe
fotocopi ya mtu fulani. Utapata tabu sana kama hujui mapenzi ya Mungu kwako.
Mungu
anaweza kuruhusu maisha fulani kwako kwa sababu fulani.
Waefeso 5:10 “mkihakiki
ni nini impendezayo Bwana.(finding out what is acceptable to the Lord)”
Waefeso 5:17 “Kwa sababu hiyo msiwe
wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.”
1 Yohana 5:14 “Na
huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi
yake, atusikia.”
Tunawezaje
kuyajua mapenzi ya Mungu
1.
Kusoma na kuelewa Neno Lake
Mathayo 7:21 “Si
kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali
ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”
Zaburi 119:105 “Neno
lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”
Neno linalokujia kwa uvuvio bila kupingana na maandiko
matakatifu (Neno la Bwana likanijia kusema…). Hakuna andiko linalotaja umuoe
fulani au uolewe na fulani. Ila huwezi kupewa neno la kuoa mke wa mtu, kuishi
bila utaratibu nk.
2.
Kugeuzwa kwa kufanywa upya nia (mindset) = metamorphosed
Rum 12:2 “Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
3. Kumuomba Mungu na
kumsubiri
Luka 22:42 “akisema,
Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi
yangu, bali yako yatendeke.”
Mfano: Paulo: 2 Kor 12:7-10 “Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.”
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unipe neno la kinabii la kuniongoza
katika maisha yangu ili nisitafute maisha ambayo hujanipangia.
2. Ee Mungu naomba unifundishe kuomba na kuwa na subira ili
nisipishane na majibu yako.
3. Ee Mungu naomba usafishe akili yangu ili niweze kujua
mapenzi yako kwangu.