Ticker

6/recent/ticker-posts

JIFUNZE KUISHI MAISHA YA IMANI (Soma maandishi na kuangalia video fupi)

Jifunze kuishi maisha ya imani (Bofya hapa uangalie video)

JIFUNZE KUISHI MAISHA YA IMANI (Soma maandishi na kuangalia video fupi)

Watu wengi wanatamka kwa kinywa kwamba wanamuamini Mungu lakini kivitendo wako tofauti kabisa.

Maana ya imani: Ebr 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Lazima upate UHAKIKA MOYONI KWA WAZI KABISA INGAWA KIMWILI HUJAPOKEA BADO.

Ukisoma Waebrani 11 utagundua kwamba imani inajulikana kwa matendo yake. Lazima UCHUKUE HATUA YA IMANI.

“Kwa imani” ni neno linalojirudia mara 18 hivi.

Mst 30 “Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba.”

Mtu anayekuambia uamini tu utapata pesa anakudanganya. Mwambie akupe kazi ya kufanya au akuombee upate kazi lakini na wewe utafute kuwa na vigezo pia.

Marko 11:20-23 “Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

Maombi ya wiki hii:

1. Ee Mungu naomba unipe imani ya kweli nisitengeneze ya kwangu mwenyewe isiyo na matokeo.

2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuchukua hatua ya imani katika yale ninayoamini ili yaweze kutokea. Niwe na action plan.

Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya mtandao). Pia unaweza kuingia kwa urahisi katika majukwaa ya huduma hii yaliyoko Facebook, Tiktok, Youtube, Soundcloud, Whatsap na Blog ukidownload na kuinstall App ya LAWI MSHANA