EPUKA MISAADA KUTOKA KWA MAWAKALA WA SHETANI (Bofya hapa uangalie video)
EPUKA
MISAADA KUTOKA KWA MAWAKALA WA SHETANI
Mawakala wa shetani hawawezi kukupa fedha bure. Lazima
utatumikishwa katika eneo fulani. Shetani hawezi kamwe kumpa mtu kitu cha bure
au ‘uhuru.’
1. Msaada
wa shetani unaambatana na kumsujudia
Lk 4:6-8 “Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.”
2. Msaada wa shetani sio wa kudumu na kuna dhuluma ndani yake
Mit 8:18 “Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.” (Riches and honor are with me, Enduring riches and righteousness.)
Sifa za utajiri usiotoka kwa Mungu:
1 Tim 6:9,17-19 “9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. 18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; 19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.”
1. Msukumo wake ni tamaa na sio kutimiza
mahitaji (kuwa na vitu ambavyo sio
mahitaji yako) – desire to be rich
2. Ni wa kujionyesha au kujikweza – waagize wasijivune
3. Hauna uhakika (sio yakini) – masharti magumu
4. Huufurahii (unaweza kumiliki nyumba lakini huruhusiwi kulala ndani) – furahia
unachomiliki!
5. Unaupata kwa kumdhulumu au
kumnyang’anga haki mtu fulani – wawe
matajiri kwa kutenda mema
6. Ni vigumu kuwasaidia wengine kwa moyo (labda pale tu anapotaka kujionyesha au
kujitangaza) – familia ina shida ila anajionyesha mitandaoni au kukupa vitu vya
kukuathiri kv pombe – wawe tayari kutoa mali zao kwa moyo
7. Hauchangii kazi ya ufalme wa Mungu (hafikirii kwamba kuna maisha mengine yanayohitaji
kuwekeza na sio benki peke yake) – waiwekee akiba kwa wakati ujao ili wapate
uzima wa milele. (that they may lay hold on eternal life.)
Maombi ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba unisaidie nishinde vishawishi vya kupata
kazi au mali kwa kumsujudia shetani
2. Ee Mungu naomba niwe radhi na baraka zangu na nifanikiwe katika maisha yangu kwa njia ya haki ili nisije nikapoteza roho yangu.
Unaweza ku-download na ku-install App ya LAWI MSHANA ambayo ipo kwenye blog hii.