KWA NINI UNAMTOLEA MUNGU VIZURI LAKINI BADO MAISHA NI MAGUMU (Bofya hapa uangalie video)
KWA
NINI UNAMTOLEA MUNGU VIZURI LAKINI BADO MAISHA NI MAGUMU
1.
Huzingatii kanuni za uchumi wa ki-Mungu
(i) Bidii ya kazi: Ruthu 2:5-7 “Kisha Boazi akamwuliza mtumishi aliyewasimamia wavunaji, Na huyu je! Ni msichana wa nani? Yule msimamizi aliyewasimamia wavunaji akajibu, akasema, Ni yule msichana Mmoabi aliyerudi pamoja na Naomi, kutoka nchi ya Moabu; naye akasema, Tafadhali niruhusu kuokota masazo, na kukusanya nyuma ya wavunaji kati ya miganda; basi akaja, naye ameshinda tangu asubuhi hata sasa, isipokuwa alikaa nyumbani kitambo kidogo”
Ruthu aliinuliwa kwa sababu ya bidii ya kazi. Huyu binti Mmoabu akaolewa na tajiri ambaye alikuwa ni mmiliki wa shamba hilo.
Mithali 22:29 “Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.” (Do you see a man who excels in his work? He will stand before kings; He will not stand before unknown men.)
(ii) Matumizi
mazuri: Tito 3:14 “Watu wetu nao wajifunze kudumu
katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo
lazima, ili wasiwe hawana matunda.”
Tusiombe tu kubarikiwa bali tuombe pia Mungu atufundishe
kuwa na matumizi mazuri.
(iii) Kuweka akiba: Mit 6:6-8 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”
Akiba ni muhimu kwa watu wote yaani, matajiri na maskini. Lakini pia ni agizo la Mungu kwamba tusishindwe na sisimizi wanaoweka akiba.
2. Maisha
ya laana kwa kutomtii Mungu
Kum 28:43-45 “Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini. Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia. Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza.” (….all these curses shall come upon you and pursue and overtake you….)
Unaposhindwa kutii maagizo uliyoambiwa na Mungu, unafungua mlango wa kuishi maisha ya laana.
3. Unatoa sadaka katika madhabahu zisizo sahihi
Kum
12:13 “Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa
katika kila mahali upaonapo.”
Kuna madhabahu zinakuunganisha na shetani badala ya
kukuunganisha na Mungu. Usiulize jina la mchungaji wala jina la dhehebu, ULIZA
JINA LA MADHABAHU.
4. Unakula
vyakula na sadaka za kishetani
1 Kor 10:20,21 “Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.”
Unashiriki sherehe za kishetani. Hoji kila mwaliko unaopewa.
Kut
34:15 “Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu
wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja
akakuita, ukaila sadaka yake.”
Matajiri wanapotoa sadaka kwa miungu wanatakiwa kuwalisha
watu fulani ili wawatawale vizuri kiuchumi
Maombi
ya wiki hii:
1. Ee Mungu naomba uniwezeshe kuzingatia kanuni za uchumi
wako ili nisiombe tu bila kuzifanyia kazi.
2. Ee Mungu naomba uniwezeshe kusikiliza sauti yako na
kufanya maagizo yako ili nisiishi maisha ya laana.
3. Ee Mungu naomba unifunulie madhabahu sahihi ya kutolea
sadaka yangu ili nisiingizwe katika maagano ya kishetani.
4. Ee Mungu naomba uniepushe na vyakula vya mapepo ambayo
haviwezi kutakaswa bali vinatakiwa kutupwa.
Lawi Mshana, 0712-924234 (ushauri na maombezi kwa njia ya
mtandao).
Pia unaweza kusikiliza na kuangalia nyimbo za Injili za mke
wangu kupitia App ya LAWI MSHANA. Unaweza kuidownload kupitia Blog hii.
Hivi karibuni utaweza kuangalia nyimbo za Album yake mpya
kupitia App hii. Download, install na ku-share kwa wengine pia.

